2015-01-10 08:42:51

Diplomasia inaendelea kuimarika kati ya USA na Cuba!


Serikali za Marekani na Cuba zinaendelea kuimarisha mahusiano yao ya kidiplomasia baada ya kukata mzizi wa fitina uliotawala nchi hizi mbili kwa kipindi cha miaka hamsini na tatu. Ujumbe kutoka Serikali ya Marekani unatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa Cuba kuanzia tarehe 21 hadi tarehe 22 Januari 2015.

Mkutano huu pamoja na mambo mengine unapania kuweka msingi wa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, kama yalivyoasisiwa na Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Raul Castro wa Cuba. Wahamiaji, wafungwa wa kisiasa walioko Cuba ni kati ya mambo yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo. Baadhi ya wafungwa wa kisiasa tayari wamekwishaachiliwa, kama sehemu ya mchakato wa maridhiano ya kidiplomasia.







All the contents on this site are copyrighted ©.