Hakuna kinachoweza kuhalalisha kitendo cha kuondoa maisha ya mtu
Baada ya kusikia habari ya mashambulizi ya kutisha yaliyofanyika Paris katika makao
makuu ya Gazeti la kila wiki la 'Charlie Hebdo' lililosababisha watu kadha kupoteza
maisha na majeruhi wengi, Papa Francisko, amejiunga katika maombi, kuombea kafara
wa tukio hili na familia nyingi zilizoumizwa na msiba huu.
Katibu wa Vatican,
Kardinali Pietro Parolin, kwa niaba ya Papa , amepeleka salaam za rambirambi za Papa
kwa wahanga wa tukio hili, ambamo amewakabidhi waathiriwa katika huruma ya Mungu,
na kuomba awapokea katika mwanga wake.Na pia anaombea familia zao na majeruhi, wajaliwe
faraja za Bwana wakati huu wa mtihani mkubwa.
Baba Mtakatifu analaani, kwa
mara nyingine tena, vurugu zenye kusababisha mateso mengi na kumwomba Mungu zawadi
ya amani, na kuzitakia familia zilizoathirika zaidi, baraka ya Mungu.
Pia
Msemaji wa Vatican, Padre Federico Lombardi, ameviambia vyombo vya habari kwamba,
Baba Mtakatifu, analaani vikali shambulio hili la kuchukiza, uhalifu uliotikisa
si tu watu wenye mapenzi mema Ufaransa, lakini duniani kote.
Na kwamba, Papa
Francisco anatolea zake sala na kushiriki mateso ya kafara, majeruhi na familia kutokana
na uhalifu huu , hasa mateso ya familia za mateso ya waliojeruhiwa na familia ya
watu waliokufa, na juu ya yote, ametoa wito wa kupinga kwa njia zote, uenezaji wa
chuki na aina zote za unyanyasaji, kimwili na kimaadili, ambavyo huharibu maisha ya
binadamu, utendaji wowote wenye kukiuka hadhi ya watu, na wenye kuathiri kwa kiasi
kikubwa, msingi ya amani na mshikamano mzuri kati ya watu, licha ya tofauti za
utaifa, dini na utamaduni.
Hakuna kinachoweza kuhalalisha vurugu zenye mauaji.
Mauaji ni adui wa mawazo, na kamwe hayawezi kuhalalishwa kwa kuwa maisha ni heshima
ya kila mtu na yanapaswa kulindwa kwa uhakika dhidi ya maamuzi yoyote yaliyo kinyume
, yoyote yanayo weza kuleta chuki. Ni lazima kukataa mauaji. Ni lazima kuheshimu
maisha na kuyalinda. Papaa ameonyesha ukaribu wake na mshikamano wake wa kiroho
na msaada kwa wale wote ambao, kwa mujibu wa majukumu yao mbalimbali, wanaendelea
kufanya kazi, kwa ajili ya amani, haki na sheria, uponyaji wa kina wa vyanzo na saba
bu zinazoweza kujenga chuki, kama ilivyoonekana sasa Ufaransa na duniani kote kwenye
dalili za mvutano na vurugu. Pia Maaskofu Katoliki wa Ufaransa wametoa tamko lao
kufuatia shambulio hili katika jengo la gazeti la Charlie Hebdo, wakisema, “ kitendo
hiki ni cha kufedhehesha na si haki”. Maaskofu wa Ufaransa wamelaani kwa nguvu unyama
huu na kutoa wito kwa serikali kuwapata wahusika wote na kuwafikisha mbele ya sheria.
Katibu na msemaji wa Maaskofu, Ribadeau Olivier Dumas, ameonyesha hofu ya Maaskofu
kwa kile kilichotokea na kwamba wote watakuwa karibu jamaa wa waathirika na wafanyakazi
wa gazeti hilo. Na kwamba hakuna kinachoweza kuhalalisha vurugu hizo, ambazo
huathiri uhuru wa kujieleza, msingi muhimu wa jamii ya Ufaransa. Na pia wamewataka
wananchi wasitende kwa ghadhabu za kulipiza kisasi , lakini wauishi msiba huu kwa
kujenga udugu na mshikamano , kama vipengere muhimu katika udumishaji wa amani .