2015-01-05 12:41:34

Uteuzi wa Makardinali wapya umezingatia kigezo cha Kanisa la Ulimwengu- Padre Lombardi


Msemaji mkuu wa Vatican, Padre Federico Lombardi, kwa muhtasari ametoa ufafanuzi juu ya uteuzi wa Makadinali wapya , akisema kwamba, uteuzi mpya uliofanyika, umeweza kuziba pengo la makardinali 12 lilillo kuwepo katika idadi ya Makardinali 120 wapiga kura. Papa Francisko ameongeza kidogo idadi hiyo.

Katika uteuzi huu, kigezo cha wazi kinachoonekana, ni umoja wa kanisa katika mapana ya kanisa Katoliki la ulimwengu. Kuna wateule wapiga kura wapya , kutoka nchi 14 tofauti, kati yake sita, ikiwa ni kutoka katika nchi ambazo hazikuwa hata na Kardinali mmoja na baadhi ikiwa ni mara ya kwanza kuwa na Kardinali. Na kwa kujumisha na majina mengine matano mapya mateule, ambao ni Maaskofu wastaafu , uteuzi mpya unawalikisha mataifa 18.

Katika uteuzi huiu, kwenye kundi la wenye haki ya kupiga kura, kuna watano kutoka bara la Ulaya, Asia watatu , Amerika ya Kusini watatu , wawili Afrika na wawili Oceania. Hakuna Makardinali wapya wateule kutoka Amerika ya Kaskazini (Marekani na Canada) kwa sababu idadi yao ni tayari ni kubwa na hivyo imebaki kama ilivyokuwa mwaka jana.
Padre Federico Lombardi ametaja mataifa yaliyopata Kardinali kwa mara ya kwanza ni Cape Verde, Tonga, Myanmar , ambako kuna jumuiya ndogo ndogo za kanisa au kuwa kati ya nchi zenye waamini wachache. Askofu wa Tonga ni Rais wa Baraza la Maaskofu linalo unganisha Maaskofu katika visiwa vya Pasifiki. Dayosisi ya Santiago de Capo Verde ni moja ya majimbo Katoliki makongwe ya Afrika, na Jimbo la Morelia Mexico ni kati ya mikoa ya Mexico yenye kusumbuliwa vurugu za kijamii. Na kwamba, kuna kardinali mteule mmoja tu kutoka Idara za Curia ya Roma, ambao kwa sasa ni juu kidogo tu ya robo ya Makardinali wenye dhamana ya kupiga kura.

Aliendelea kusema, ni hii inaonyesha wazi kwamba, Papa habaki amefungwa na utamaduni wa kale katika uteuzi wa Makardinali, ambao awali zaidi ulimotishwa na sababu za kihistoria katika nchi mbalimbali - ambamo Kardinali ilionekana kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Idara husika. Lakini sasa badala yake kuna majina mbalimbali ya Maaskofu Wakuu na maaskofu, ambayo awali hayakuwahi kna uhusiano na Kardinali.

Aidha Padre Lombardi amezungumzia juu ya uteuzi wa wastaafu , akisema, Papa ameonyesha kutambua utendaji wa wastaafu hao kama alivyoeleza kwa kifupi katika utangulizi wake, kwamba, wao wanakilisha Maaskofu wengi ambao, pamoja na huduma hiyo kama wachungaji wa Jimbo, pia walihudumu katika ofisi za Curia na huduma za kidiplomasia. Kuteuliwa kama Kardinali, kuna lenga kuonyesha kutambua juhudi na kazi za baadhi ya watendaji, kama mfano bora wa kuigwa na wote.

Katika uteuzi huu, Kardinali mteule mpya mwenye umri mdogo zaidi ni Askofu Mkuu Tonga, Mons. Mafi aliyezaliwa mwaka 1961, ambaye anakuwa pia Kardinali mwenye umri mdogo zaidi katika dekania nzima ya Chuo cha Makardinali. Na Kardinali mkongwe zaidi ni Askofu Mstaafu wa Manizales, Mons. Pimiento Rodríguez, 1919.








All the contents on this site are copyrighted ©.