Baba Mtakatifu Francisko anahimiza, wakati huu wa mapambazuko ya mwaka mpya, ni wakati
wa kuwasha ndani ya mioyo, matumaini mapya ya imani, kwa ajili ya kuwa wajenzi
wa amani, mahali popote, siku hadi siku. Papa alitoa himizo hilo wakati wa sala ya
Malaika wa Bwana, siku ya Jumapili, ambamo alirudia kusema kwamba, daima kuna uwezekano
wa kuelewana, ingawa inaweza kuwa kazi ngumu kwa wale waliobobea katika utendaji
wa giza nene la kutengeneza vita.
Papa alieleza akionyesha imani yake kali
kwamba, daima kuna mwanya wa maridhiano, hata kama maneno ya mwanga na amani, wakati
mwingi humwezwa na hali halisi za wale wanaopendelea giza la maovu na vita. Papa
Francisco alirudia kusema maneno hayo, akiendeleleza mafundisho yake, juu ya mwanga
na amani, kama alivyoeleza pia katika ujumbe wake wa tarehe Mosi Januari, ambayo
ni Siku ya kuombea amani duniani. Maelezo ya Papa, yalizielekea taarifa za ghasia
na machafuko zinazotolewa kwa wingi kila siku katika vyombo vya habari vya Kimataifa
na kitaifa pia kama vile, amani haiwezi kupatikana bila kuwa na ghasia na vita au
bila ya kunyamazisha bunduki. Papa anasema, inawezekana kabisa kuepuka hali hiyo
na kuwa na mwanzo mpya wa kutembea katika njia ya mafanikio ya amani kupitia utendaji
mbalimbali .
Papa alieleza akiifikiria migogoro mbalimbali yenye kusababisha
umwagaji damu katika mikoa mingi duniani , msuguano katika familia na jamii, na hata
katika baadhi ya Parokia, mna vita! Na pia alipeleka mawazo yake katika miji mingi
ya dunia na nchi kati ya makundi ya vyama mbalimbali ya kitamaduni kikabila na kidini.
Papa alitahadharisha kwamba, tunahitaji kujua, licha ya upinzani wote kwamba, maelewano,
mara zote huwezekana, katika kila ngazi na katika kila hali. Na kwamba hakuna ustawi
bora kwa siku za baadaye bila kuwa na amani .
Papa alieleza na kurejea kiini
cha Ujumbe wa Injili ya siku kutoka Injili ya Yohana, pia akiangalisha katika mazingira
ya hali ya hewa ya siku ya Jumapili ilivyokuwa katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro, ambako maelfu kwa maelfu ya watu walikuwa wamefurika kumsikiliza , na hivyo
aliendelea kuzungumzia tofauti ya mwanga na giza, na kukemea unafiki mkubwa wenye
kuangamiza watu wengi duniani , kutokana na kukosekana kwa amani duniani.
Alisema,
watu huzungumzia juu ya mwanga, lakini wakati huohuo wakipendelea utulivu kudanganyifu
wa giza. Mara kwa mara huzungumzia amani lakini wakati huohuo wakichagua vita au kufanya
kosa la kukaa kimya, bila jitihada zozote halisi za kujenga amani (...) Kwa kweli
, Papa alisisitiza, “Mtu yeyote atendae maovu anauchukia mwanga! Na hatoki katika
mwanga kwa kuwa matendo yake si ya mwanga. Atendaye maovu anauchukia amani. "
Papa
alieleza kwa kuangalisha pia katika ujumbe wake, alioutoa kwa ajili ya Siku ya Kuombea
Amani duniani hapo tarehe Mosi Januari , ambao kwa mwaka huu umeongozwa na Madambiu
: Hakuna Mtumwa, sote ni ndugu. Mada iliyofungamana katika moyo wa Papa Francisko,
ambaye ameonyesha hamu yake katika kila hali, kiloa mtu auanze mwaka mpya na matumaini
mapya sehemu zote duniani, kw akuwa na umoja na muungano kamili uliosimikwa katika
moyo wa kuheshimiana, haki na upendo.
Papa anakemea kila aina ya unyonyaji
katika maisha yote ya kaijamii akisema , ni unyonyaji ni maovu y yanayo dharirisha
mahusiano ya kijamii. Kila mtu wa kila jamii, anayo njaa na kiu kwa ajili ya amani,
hivyo ni muhimu tena ni dharura, kujenga amani. Fanyeni amani kila mahali. Katika
mzizi wa amani kuna sala, Ni wito wa Papa hasa Wakristo kutenda ipasavyo. Ni lazima
kuiomba zawadi hii. Ni lazima kila siku kudhamiria hili.
Alfajiri ya mwaka
huu mpya, sisi wote tumeitwa kufufua mapigo ya moyo katika matumaini. Lakini hatuwezi
kutenda vizuri katika hili , iwapo hakuna amani tangu nyumbani kwako na katika
jamii yako, kazini, safari, na pengine pote ni kufanya amani! Papa anasema hii ni
ishara ndogo lakini ya thamani sana. Inaweza kuwagawia wengine mbegu hii ya amani,
mbegu ya matumaini, yenye kufungua barabara ya matarajio ya amani.