2014-12-29 14:45:40

Kiongozi wa Kiroho wa Waisrael Waafrika Wayahudi afariki dunia.


Yerusalemu -Kiongozi wa kiroho wa Wamarekani Weusi, wanaodai asili yao ni Wayahudi Weusi wa Israel wa kabila la Yuda la tangu Israel ya kale, amefariki dunia katika mji wa Dimona, Kusini mwa Israel , ambako alihamia miaka 40 iliyopita toka Marekani.

Msemaji wa kikundi hicho , ametaarifu kifo cha kiongozi wao Ben Ammi Ben Israel, kwamba kilitokea siku ya Jumamosi, akiwa na umri wa miaka 75, na alizaliwa huko Chicago mwaka 1939.

Ben Ammi Ben Israel, alisisitiza kuwa wao ni Wamarekani weusi, lakini ni uzao wa kabila la Yuda linalotajwa katika kitabu Kitakatifu cha Biblia. Na kwamba, wahenga wao walihamia Afrika Magharibi, baada ya Wayahudi kuharibu hekalu la Yerusalemu mwaka 70 AD, na baadaye uzao wao uliuzwa kama watumwa Marekani. Mwaka 1966, Ben Ammi, alidai kupata maono kutoka kwa malaika Gabriel aliyemwambia `` kurudi katika nchi takatifu kwa njia waliyokuja nayo ya ' Yafah Baht Gavriel.

Ben baada ya jozi hizo, aliwakusanya wafuasi wake wengi wakiwa mjini Chicago , na kuwaongoza hadi Liberia Afrika Magharibi taifa lililoteuliwa kuwa nchi huru kwa watumwa kunako karne ya 19. Na walihamia Israel mwaka 1969 na kutengeneza makazi yao, eneo la Dimona, mji wa Kusini wenye kuwa na umaskini mkubwa wa kukithiri katika eneo la jangwa la Negev jangwa, ambako kunatajwa kuwa mlango wa kuingilia wahamiaji haramu . Ben Ammi amejulikana kwamba alikuwa na mapenzi makubwa kwa nchi ya Israeli, ambako alitengeneza makao ya maisha yake yote, kwa imani kwamba, ni nchi yake ya asili kama mzawa mwenye damu ya kiebrania.

Pia inaelezwa kundi hili la Wayahudi weusi , limekataa kuongekea dini ya Kiyahudi, hata kama ni moja ya sharti la kupata haki ya kuwa raia wa Israel na ingawa wanaamini kuwa na damu ya Wayahudi wa kweli wa Israeli ya tangu kale. Maisha yao yanafuata misingi ya Torati na mafundisho Ben Israeli, lakini bila kuwana jadi zinazo fanana na Uyahudi zinazofundishwa na Walimuw a dini ya Kiyahudi "Marabbi".

Kundi hili linajulikana kwa mavazi yake yenye rangi za mg’ao , kuuoa wake wengi , kuzaa watoto wengi, , hawali nyama wala maziwa ya wanyama, mayai au kitu kilicho tengenezwa na sukari . Jumuiya hii, ina maelfu ya wafuasi, wengi wao wakiwa Marekani, visiwa vya Carribbean na Afrika Magharibi. Na wengi wao husema maisha yao wameyatolea kumtumikia Yahweh au Mungu. Na huitana kati yao Mtakatifu.

Serikali ya Israeli, ikiwa haina uhakika na madai ya watu hao, haijui nini la kufanya kwa wageni hao , ambao wana majina ya Kiebrania, lakini mtindo wa mila zao ni za Afrika Magharibi, hasa baada ya Israel kutangaza sheria ya kutoa uraia, kwa watu wote wanaodai kuwa na asili ya Israel.
All the contents on this site are copyrighted ©.