Tabia ya kusherehekea misa tatu na masomo yake – ina maana yake. Kesha: huadhimisha
kuzaliwa kwa Bwana na mwokozi – kabla ya nyota nilikuzaa – toka tumbo la Baba. Ni
kutangaza Bwana amezaliwa. Wale waliomngoja Bwana katika majilio na wale wanaomsubiri
kama mamajusi wanasikia sauti hiyo.
Sherehe iliyojulikana ya kwanza mwaka
336 –baada ya miaka 100 – wakristo wote karibu walirithi tabia hii – chanzo maandiko
matakatifu – angalia Injili ya leo. Kwa kuja kwake wakovu umekuja duniani.
Isaya
anatupa picha ya mwana mfalme anayezaliwa. Tangu hapo – Isaya anaona uzao huo = ushindi
wa Mungu dhidi ya adui zake. Hali hii haikutokea wakati wa uhai wake –sifa juu ya
mtoto huyu - amani na haki ya milele - inatuonyesha wazi kuwa Yesu ndiye huyo mwana.
Hakika ndiye huyu mshauri wa ajabu, Mungu mkuu, Mungu daima, Mfalme wa amani. Hek.
18:14-15 – ukimya mzito kabisa ulipotanda na usiku mnene – Neno liliingia katikati
ya nchi.
Mwinjili Luka anatushikisha utabiri huo wa nabii Isaya. Aidha kadiri
ya Isaya mtoto huyu angeonekana – kuja kwa kishindo. Katika Injili ya Luka - siyo.
Alizaliwa katika hori- pango. Hakika siyo rahisi kuamini ukuu wake. Luka alikuwa na
imani hiyo–tangazo la malaika kwamba huyo ni masiha na Bwana na nyimbo – utukufu kwa
Mungu juu …… unakamilisha imani hiyo. Ile iliyokuwa siri - sasa imefunuliwa kwetu.
Mwinjili anatambua kuwa katika udogo huo – huyu atakuwa mfalme wa ulimwengu.
Katika
Tito – Neema ya Mungu imeonekana kwetu ambapo wokovu unawafikia watu wote. Katika
Efe. 1:5 – toka mwanzo aliazimia kutufanya watoto wake kwa ajili ya Yesu Kristo. Efe.
1:9 – ametujulisha fumbo la mapenzi yake kadiri ya azimio lake Bwana alilokusudia
katika yeye.
Tito 3:4 – uwezo wa upendo kupindua mambo – kipengele mhuri wa
tumaini la kikristo –lakini wema wa mwokoziwetu Mungu, na hisani yake kwa wanadamu
zilipotokea, ametuokoa – si kwa matendo yetu ….isipokuwa kwa huruma yake.
Hivyo
Noeli – ni ufunuo wa juu kabisa wa Mungu – upendo wake kwa wanadamu – mapenzi ya Mungu
na upendo wake kwa wanadamu vyaonekana wazi – Tito 3:4. Sisi tunaalikwa kuishi
mapenzi hayo na upendo huo hapa duniani. Wajibu wetu ni kueneza mapendo na haki, kuachana
na kila aina ya ubaya na uovu.
Angalisho: wale waliopata taarifa wa kwanza
wachungaji waliofunga safari – mamajusi –wanatuambia nini leo katika maisha yetu ya
ufuasi/imani? Tunapoadhimisha Noeli tena leo? Ni moyo mnyenyekevu tu unaoweza kutambua
na kupokea mambo haya –angalia wachungaji wanasikia malaika wakiimba – utukufu kwa
Mungu juu – ni nani hao wenye mapenzi mema?
Mungu amejifanya mtu ili tuweze
kumwona – vinginevyo Mungu wetu angebaki mbali – wa kusikika sikika tu. Akajifanya
mtu, akawa mtoto – ili sisi tumkaribie Mungu –chombo cha amani na upatanisho. Nasi
leo tuna furaha kuimba pamoja na mwinjili Luka 2:14 – utukufu kwa Mungu juu katika
maisha yetu.
Asubuhi ya Noeli
Isa. 62:11-12, Tito. 3:4-7,
Lk. 2:15-20 Misa yatangaza mwanga wa ulimwengu – kuzaliwa toka tumbo la Maria.
Kanisa laadhimisha mapambazuko ya matumaini mapya ya mwanadamu. Mwanzo mpya. Tunaona
furaha ya Isaya, ya Tito – maisha ya milele, ya wachungaji. Watu wa kawaida wanaonekana
katika pango alipozaliwa Yesu.
Somo la Isaya – lazungumzia ujio wa mwokozi
mwishoni mwa utumwa wa Babeli. Wamejitoa katika utumwa – wanaitwa watakatifu – tofauti
na watu wa mataifa – wanarudia hali yao ya zamani – watoto wa Mungu. Hata hivyo –
Isaya anazungumzia ukombozi ulio zaidi ya mwili = unabii huu – unakamilika katika
sherehe hii ya leo – ukombozi wa kweli toka kwa mtoto aliyezaliwa leo.
Wachungaji
wanaenda kutangaza habari hiyo njema – mwokozi amezaliwa Habari hii njema – iko wazi
katika somo la pili - Yesu ndiye huyo mwokozi. Yuko kati yetu. Mkristo aliyejaa Roho
Mtakatifu– anabatizwa katika mwili wa Kristo – Kanisa – na anaendelea kutangaza habari
hiyo njema - 1 Pt. 2:9-10. Uwepo wa Kristo = mapambazuko kwetu sisi – wokovu na ubatizo
na Roho Mtakatifu – Ef. 5,26.
Hivyo Habari Njema ndiyo hii, Bwana amezaliwa
kati yetu. Upendo na uzuri wa Mungu = Kristo. Tito – Kristo – zawadi ya Mungu kwetu
- siyo siri tena. Mungu amejifanya mtu akakaa kati yetu – Mt. 1,23. Hiyo zawadi –
sisi tunakuwa warithi na uzima wa milele. Mapambazuko haya ya matumaini yanashangaza.
Isaya anamtumaini Mungu, Maria anayeweka katika moyo wake, wa wachungaji wanatangaza
habari hiyo njema – utukufu wa Mungu.
Kila mkristo asubuhi hii anaushangaa
ukuu wa upendo wa Mungu na kuutukuza mpango wake wa ukombozi na jinsi alivyoukamilisha
kwa ajili yetu. Tendo hili takatifu linatuwajibisha sote. Tunafanya nini katika ulimwengu
wetu wa leo? Mungu amechukua mwili ili sisi tuweze kumwona Mungu kwa macho na kushangaa
mambo hayo makuu.
Ibada ya Misa Takatifu wakati wa mchana!
Isa.
52:7-10, Ebr.1:1-6, Yoh.1:1-18 NENO AKATWAA MWILI, AKAKAA KWETU. Misa
ya mchana – husherehekea kuzaliwa kwa Kristo katika mioyo na maisha ya waamini. Sote
twajua wazi kuwa hakuna sheria wala falsafa iwezayo kumwokoa mwanadamu. Wokovu wa
kweli uko kwa Mungu aliyejifunua kwa njia ya Kristo, yeye ndiye wokovu wetu.
Tuliyoona
katika misa ya kesha, usiku, alfajiri na sasa katika misa hii – tukio la Yesu kujifanya
mtu – sambamba na tendo la uumbaji – hapo mwanzo: Mwa 1,1. Tofauti hapo, hapo mwanzo
ya Yohani iko nje ya wakati. Yohani anasisitiza utukufu wa Kristo. Neno alikuwa Mungu
– wengi walitilia mashaka – angalia kina Tomaso baada ya kuushuhudia utukufu huo
20, 28 – Bwana wangu na Mungu wangu -kinachofuata toka kwetu ni wajibu wetu, ushuhuda,
kuishi ukweli, haja ya mwanga, haya ya imani.
Huyu Neno amechukua mwili na
akaonekana kwetu katika mwili sawa na wa kwetu. Ana hali ya kimungu na ya kibinadamu.
Kwa njia yake tunapata nafasi ya kushiriki uzima wa Kimungu. Dunia– haimjui Mungu
– kadiri ya Yohani – ingawa kwa njia yake ulimwengu uliumbwa. Yohana aliandaa njia,
kwa ufunuo wa mwana wa Mungu - yeye anayetoa neema na ukweli.
Yohana anakuwa
mdogo – pia hapa malaika ni wadogo kwake Kristo. Yohani aliandaa njia –kama ilivyo
katika somo la kwanza aliongea juu ya mfalme wa haki na amani, raha na wokovu utimilifu
huu – Kristo alichukua mwili. Maandalizi ya furaha hii yamefanywa katika Ebrania –
anazungumzia juu ya wajibu wa mwana wa Mungu na uhusiano wake na mpango wa ukombozi
– juu ya uana wa Mungu, ukuhani wa Yesu na utukufu wa Bwana Yesu mfalme - hapa neno
aliyefanywa mtu ni pekee.
Hivi sasa Mungu anaongea nasi kwa njia ya mwanae
– si kwa njia ya manabii tena. Yeye ni utimilifu wa dahari. Huyu mwana ndiye sababu
ya uwepo wa ulimwengu. Ndiye utukufu wa Mungu Baba. Yesu ni mfano unaonekana wa Mungu
asiyeonekana. Anionaye mimi amemwona Baba – Yoh. 12:45. Kwa kuchukua kwake mwili,
sisi tumepata nafasi ya kumwona Mungu kwa macho yetu na hali zetu. Ni fumbo ambalo
tunaalikwa sana kuendelea kulitafakari ili pole pole aendelea kujifunua kwetu kadiri
tunavyoendelea kuungana naye.
Ebr. 2,14 – Yesu ni Mungu, ni mwana wa Mungu,
ni Mungu, ni mtu. Noeli – sherehe ya pekee na ya fumbo la pekee - Mungu amezaliwa
kwetu – ni juu ya Noeli – sherehe ya pekee na ya fumbo la pekee – Mungu amezaliwa
kwetu – ni juu ya yote, ndiye ukamilifu wa yote – aliyetangazwa na Isaya, akatangazwa
na Yohani Mbatizaji na akazaliwa kwetu. Anashiriki ubindadamu wetu. Anakuja kwetu
na analeta ukombozi. Lengo ni kuunganisha watu wote katika jamii moja. Kwa fumbo hili
tunaruka hatua mbele katika ukombozi wetu. Tunamkaribia Mungu. Matumaini yanafunguka
na milango ya mbingu inafunguliwa.
Papa leo Mkuu anasema - mtu afurahi kwa
kuwa anaikaribia taji ya ushindi. Mtu mwenye dhambi yeye naye afurahi kwa kuwa anasamehewa
dhambi zake na mpagani sharti afurahi kwa kuwa anaitwa kupewa uzima.