2014-12-24 10:37:38

Noeli, iwe ni mwanzo mpya wa kuchuchumilia utakatifu wa maisha!


Askofu Josefu Mlola wa Jimbo Katoliki Kigoma, Tanzania katika maadhimisho ya Siku kuu ya Noeli, kupitia Studio za Radio Vatican anapenda kuitakia Familia ya Mungu, heri na baraka kwa Siku kuu ya Noeli, Yesu Kristo, Mkombozi wa dunia azaliwe tena mioyoni mwao! Familia zijitahidi kuhakikisha kwamba, Yesu Kristo anapata nafasi katika maisha na utume wao, hali kadhalika kwa Familia yote ya Mungu. RealAudioMP3

Askofu Mlola anakazia nafasi ya familia katika Siku kuu hii ya Noeli kutokana na mkazo unaoendelea kutolewa na Baba Mtakatifu Francisko, ili kujenga na kuimarisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia, ili Kanisa liweze kuwa tayari kuwatangazia Watu wa Mataifa Injili ya Familia inayojikita katika upendo mkamilifu kati ya Bwana na Bibi, Uaminifu, Udumifu, Msamaha na Utakatifu wa maisha.

Askofu Mlola anasema, Mtoto Yesu awakirimie wanafamilia wote maisha mpaya, ili kweli Noeli hii iweze kuwa ya kwanza, ya pekee pengine na ya mwisho kanisa katika hija ya maisha yao hapa duniani. Noeli ya Mwaka 2014, uwe ni mwanzo mpya kwa waamini kuchuchumilia utakatifu wa maisha, kwa kutambua kwamba, huu ni wito wa kwanza kwa kila Mkristo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.All the contents on this site are copyrighted ©.