Baba Mtakatifu Francisko , Jumanne wiki hii, amepeleka barua ya matashi mema ya
Siku Kuu ya Noeli kwa Wakristo wa Mashariki ya Kati, akionyesha ukaribu wake katika
wakati huu, ambamo Wakristo wanahangaishwa na ukatili na ghasia za zinazoendelea
katika mkoa huo, hasa ghasia zinazojirudia mara kwa mara, zinazofanywa na makundi
ya kigaidi.
Papa ameonyesha kuungana na Wakristo hao katika mateso yao na
shida zao kutokana na ukosefu wa amani. Amesema, yeye kila siku , hufuatilia taarifa
mpya za mateso makubwa yanayo jirudiarudia kwa watu wengi katika Mashariki ya Kati.
Na hasa kwa namna ya kipekee kwa watoto, akina mama vijana, wazee, na wakimbizi
wote, na wale wote wanaokabiliwa na njaa na kukabiliana na uwepo wa baridi kubwa
, bila makazi.
Papa ameandika , katika hali hii ya mateso ya watu hao, ni
vigumu kwake kukaa kimya wakati sehemu ya mwili wa Kristo inaumizwa na ukatili wa
binadamu. Hivyo anamlilia Mungu, kupitia dhamira na sala zake, Mungu awezeshe uwepo
wa juhudi thabiti za kusaidia kwa njia yoyote, ili amani irejee tena kwa wote, na
pia ameonyesha ukaribu wake binafsi na mshikamano, kama vile ilivyo kwa Kanisa zima
la Ulimwengu kwa kuwapa neno la faraja na matumaini.
Papa kwa namna ya pekee,
ametoa salaam na heshima zake kwa viongozi wa Kanisa wote, Mapatriaki, Maaskofu,
Mapadre, Watawa wanaume na wanawake, ambao wanaongoza jamii ya Kanisa Mashariki
ya Kati , kwa upendo na kujitolea sadaka, licha ya hali hizo za wasiwasi na mateso
makubwa. Papa ametaja thamani ya uwepo wao , na kazi ya wale ambao wameweka maisha
yao wakfu kwa ajili ya Bwana, kumtumikia kupitia ndugu zao na dada zao , hasa wahitaji
zaidi katika yote mawili kiroho na kimwili pia, na hivyo, unakuwa ni ushuhuda wa
upendo wake usio kifani! Papa ametaja jinsi uwepo wao ulivyo muhimu katikati ya makundi
yao, hasa katika nyakati za shida! Aidha amewakumbuka vijana akisema anawakumbatia
kwa upendo wa kibaba. Amewataka wawe aminifu katika wito wao , na maendeleo yako
ya kibinadamu na Wakristo, na kufikia matumaini na ndoto zao. Na pia ametoa heshima
zake kwa wazee akisema kumbukumbu zao ni heshima kubwa kwa taifa lao.
Papa
ameendelea kuwatia moyo Wakristo wa Mashariki ya kati kwamba, uwepo wao una thamani
kubwa katika kumshudia Yesu daima, licha ya matatizo yanayowakabili. Uwepo wao una
thamani kubwa kwa ajili ya Mashariki ya Kati. Pamoja na uchache wao , lakini wana
wajibu mkubwa katika nchi hii ambamo Ukristo ulizaliwa na kuenea kwingine kote.
Wao ni kama chachu dogo. Na pia amewashukuru kwa michango yao mingi ambayo Kanisa
hutoa katika maeneo ya elimu, afya na huduma za jamii, kwa ajili ya manufaa ya watu
wote wa Mashariki ya Kati , chanzo cha utajiri wa amani katika mkoa huo. Uwepo wa
Wakristo hao ni uwepo wake pia . Na amewashukuru kwa uvumilivu wao. Papa aliendelea
kuhimiza waendelee kushirikiana na watu wa dini nyingine,Wayahudi na Waislamu, kama
ishara nyingine ya Ufalme wa Mungu, licha ya ugumu uliopo, lakini mwingiliano na majadiliano
ni muhimu. Hakuna njia nyingine ya kuwa na maelewano. Mjadala, msingi katika mtazamo
wa uwazi, katika ukweli na upendo, pia ni njia bora ya majaribu ya imani kali za kidini,
ambayo ni tishio kwa wafuasi wa dini zote. akati huo huo, mazungumzo yalenge katika
huduma ya haki na umuhimu wa amani, jambo linalofaa kukumbatiwa na wote.