2014-12-22 10:12:26

Taa za Mti wa Krismasi, ziamshe imani kwa Mungu.


(Vatican Radio) Mahujaji na wageni wanaotembelea uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika siku hizi za mwisho za kipindi na Majilio, wanafurahia pia, pambo la Mti mkubwa wa Krismasi, uliopambwa kwa taa nyingi za kuvutia, ambao taa zake ziliwashwa rasmi Ijumaa iliyopita 19 ya Desemba.

Kwa miaka mingi ya nyuma Vatican , hapakuwa na utamaduni wa kuweka mti wa Krismasi katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Lakini mwaka 1982 Papa Yohana Paulo II, alirudisha utamaduni huu wa kupamba uwanja wa Kanisa Kuu kwa mti mkubwa wa Krismasi kama ilivyokuwa utamaduni Poland, Tangu wakati huo, nchi nyingi tofauti na mikoa ya Ulaya wamekuwa wakijitolea kwa zamu kufanikisha uwepo wa pambo hili la mti wa Noel , katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro .

Mti ya mwaka huu, ambayo ni mti wenye umri wa miaka 70, umetoka katika Mkoa wa Kusini mwa Calabria, ambkyo Papa Francisco, alitembelea eneo hilo Juni mwaka huu. Katika waraka wake "Mwanga wa imaniā€ Papa Francisco, alitumia mfano wa matawi ya mti, kama jinsi imani kwa Mungu inavyoenea Taa ulimwenguni.

Mti huu wa Krismasi una urefu wa mita 25.5 kwenda juu na uzito wa tani 8, ni mti wa kuvutia kwa jinsi hata kwa jinsi shina linavyoonekana , ni shina pacha, mashina mawili tofauti yameungana pamoja na kuunda mti moja . Shina hili linatumika kama mfano kwamba, hata mwanadamu, kamwe hawezi kufanya hija ya maisha peke yake, maisha bora daima ni kuungana na Bwana. Na pambo la pango la Noel, linatazamiwa kusaidia kutoa picha halisi na maana ya tukio zima la kuzaliwa kwa mkombozi wa dunia katika maisha ya kawaida ya kijamii .
All the contents on this site are copyrighted ©.