2014-12-22 12:21:00

Kardinali Theodorè Adrien Sarr astaafu kazi za kichungaji


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kujiuzulu huduma za kichungaji za Jimbo kuu la Dakar, Senegal, lililowasilishwa na Kadinali Théodore-Adrien Sarr, kwa mujibu wa kanuni za Kanisa namba 401 § 1 katika sheria za Kanisa. Katika Nafasi yake Papa Francisko amemteua kuwa Askofu Mkuu Dakar, Askofu Benjamin Ndiaye, ambaye hadi uteuzi huu mpya alikuwa ni Askofu wa Jimbo la Kaolack.
Théodore-Adrien Sarr Kardinali, Askofu Mkuu wa sasa wa Dakar na Kardinali-Padre Mkuu wa Kanisa la Mtakatifu Lucia la Piazza d'armi Roma, alizaliwa Novemba 28, 1936, huko Fadiouth, Senegal . Alipata daraja la Upadre huko Dakaron, tarehe 28 Mei 1964. Miaka kumi baadaye, katika umri wa miaka 38, aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kaolack. Mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Dakar na kuinuliwa katika daraja la Kardinali mwaka 2007. Alitajwa kuwa Padre Kardinali tarehe 6 April, 2008.
All the contents on this site are copyrighted ©.