2014-12-20 15:16:13

Mabalozi wapya wawasilisha hati zao za utambulisho!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 20 Desemba 2014 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Jaime Bernardo anayeziwakilisha Nchi za Scandinavia mjini Vatican. Baba Mtakatifu pia amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Clelio Galassi kutoka Jamhuri ya Watu wa San Marino, moja ya nchi ndogo sana duniani.

Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Eduardo Fèlix Valdes, anayeiwakilisha Argentina mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Alhamisi, tarehe 19 Desemba 2014, Baba Mtakatifu alipokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wapya kumi na watu wanaoziwakilisha nchi zao mjini Vatican.All the contents on this site are copyrighted ©.