2014-12-20 12:17:49

Kardinali Jean-Louis Tauran ateuliwa kuwa Camerlengo mkuu


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Kardinali Jean-Louis Tauran, Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini, kuwa Camerlengo mkuu wa Kanisa Katoliki. Huyu ni kiongozi mkuu wa shughuli za Kanisa wakati kunapotokea kwamba, kiti cha Khalifa wa Mtakatifu Petro kiko wazi kwa sababu mbali mbali. Baba Mtakatifu amemteua Askofu mkuu Giampiero Gloder, Rais wa Baraza la Taasisi za Kanisa kuwa Msaidizi wa Camerlengo mkuu.

Itakumbukwa kwamba, kabla ya mabadiliko haya, Camerlengo mkuu wa Kanisa Katoliki alikuwa ni Kardinali Tarcisio Bertone ambaye alikuwa pia Katibu mkuu wa Vatican wakati wa uongozi wa Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI.







All the contents on this site are copyrighted ©.