2014-12-18 08:13:48

Tume ya kipapa ya kulinda watoto wadogo yakamilika!


Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko amekamilisha mchakato wa kuunda Tume ya Kipapa ya kulinda Watoto Wadogo yenye wajumbe 17 kutoka sehemu mbali mbali za dunia na tayari inaweza kuanza utume waka kama kawaida. Hawa ni wajumbe wenye ujuzi na taaluma: Saikolojia, afya ya akili, taalimungu, sheria za Kanisa, ualimu na tafiti za kijamii.

Kuna wanawake nane na kati yao kuna watawa wa kike wawili; wanaume ni tisa na kati yao kuna Mapadre watano. Wengine ni waathirika wa vitendo vya nyanyaso za kijinsia ambao kwa sasa wako mstari wa mbele ili kutoa majibu muafaka. Ifuatayo ni orodha ya wajumbe wa Tume hii ya Kipapa. Tume hii ina dhamana, weledi na taaluma katika mapambano dhidi ya nyanyaso za kijinsia kwa watoto wadogo. Hiki ni kielelezo makini kwamba, Kanisa linapania kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda watoto dhidi ya nyanyaso ambalo kwa sasa linaonekana kuwa ni kati ya matatizo na changamoto kubwa za kijamii.

1. Kardinali Seán O'MALLEY, OFM Cap., Rais
2. Mons. Robert OLIVER (USA), Katibu mkuu
3. Rev. Luis Manuel ALI HERRERA (Colombia)
4. Dr. Catherine BONNET (Ufaransa)
5. Marie COLLINS (Ireland)
6. Dr. Gabriel DY-LIACCO (Ufilippini)
7. Prof. Sheila the Baroness HOLLINS (Uingereza)
8. Bill KILGALLON (New Zealand)
9. Sr. Kayula Gertrude LESA, RSC (Zambia)
10. Sr. Hermenegild MAKORO, CPS (Afrika ya Kusini)
11. Kathleen McCORMACK AM (Australia)
12. Dr. Claudio PAPALE (Italia)
13. Peter SAUNDERS (Uingereza)
14. Mh. Hanna SUCHOCKA (Poland)
15. Dr. Krysten WINTER-GREEN (USA)
16. Rev. Dr. Humberto Miguel YÁÑEZ, SJ (Argentina)
17. Rev. Dr. Hans ZOLLNER, SJ (Ujerumani)

Mkutano wa Tume hii ya Kipapa utafanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 6 - 8 Februari 2015 kama ilivyokuwa imepangwa tangu awali.
All the contents on this site are copyrighted ©.