2014-12-18 14:31:38

Mabalozi ni wajenzi wa haki, amani, umoja na mshikamano wa kidugu!


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 18 Desemba 2014 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Mongolia, Bahamas, Dominica, Tanzania, Denmark, Malaysia, Rwanda, Finland, New Zealand, Mali, Togo, Bangladesh na Qatar. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwakaribisha Mabalozi wapya wanaoziwakilisha nchi zao mjini Vatican, kwa heshima na taadhima kwa wakuu wa nchi pamoja na watu wao.

Baba Mtakatifu anawatakia kheri na mema katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kweli yaweze kuzaa matunda yanayokusudiwa, kwa ajili ya kujenga na kudumisha: haki na amani; umoja, mshikamano na udugu kati ya watu. Baba Mtakatifu anasema, Jumuiya ya Kimataifa inafurahia kusikia kwamba, Serikali ya Marekani na Cuba zimerejesha tena mahusiano yao ya kidiplomasia, yaliyokuwa yamevunjika kwa zaidi ya miaka hamsini. Hii ndiyo dhamana iliyotekelezwa na Mabalozi katika mchakato wa kidiplomasia, kazi muhimu sana.All the contents on this site are copyrighted ©.