2014-12-17 12:06:45

Wahanga wa vitendo vya kigaidi wakumbukwa!


Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake kuhusu Familia, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumatano tarehe 17 Desemba 2014, amewaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuwakumbuka na kusali kwa ajili ya watu waliofariki dunia kutokana na vitendo vya kigaidi vilivyofanywa huko Sydney Australia na Pershawar, nchini Pakistan.

Baba Mtakatifu anawaombea pumziko la milele wote waliofariki katika matukio haya mawili pamoja na faraja kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa katika misiba hii. Anamwomba Mwenyezi Mungu aweze kuwaongoa na hatimaye kuachana na matendo haya yanayoendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao!All the contents on this site are copyrighted ©.