2014-12-17 11:07:54

Balozi wa Tanzania kuwasilisha hati za Utambulisho mjini Vatican


Balozi Filippo Marmo, ni kati ya Mabalozi wapya wasiokuwa wakazi wanaotarajiwa kuwasilisha hati zao za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 18 Desemba 2014. Balozi Marmo, hivi karibuni aliteuliwa na Rasi Jakaya Kikwete wa Tanzania kuwa ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Ujerumani na hivyo kadiri ya mapokeo anakuwa pia ni Balozi wa Tanzania mjini Vatican. RealAudioMP3

Akizungumza na Jumuiya ya Wanafunzi Wakatoliki Watanzania wanaosoma mjini Roma, Bwana Salvatory Mbilinyi, Afisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Italia amethibitisha kwamba, Balozi Marmo anatarajiwa kuzungumza na Makleri, Watawa na Waseminari wanaoishi Roma, hapo Jumamosi, tarehe 20 Desemba 2014. Kwa sasa mipango inaendelea kukamilishwa, ili kufahamu ni mahali gani ambapo wanaweza kukutana na kuzungumza kwa pamoja, wakati huu Balozi Marmo anapoanza utume wake kama Balozi wa Tanzania mjini Vatican.All the contents on this site are copyrighted ©.