2014-12-16 09:09:22

Zaidi ya watu 850 wameathirika kutokana na kulipuka kwa Volkano Cape Verde


Kardinali Theodore Adrien Sarr, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dakar, Senegal anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujitokeza ili kuwasaidia wananchi wa Cape Verde, walioathirika kutokana na mlipuko wa Volkano nchini humo. Anawataka waamini kutoka kila Parokia kukusanya mchango utakaopelekwa nchini Cape Verde, ili kusaidia juhudi za kuokoa maisha ya watu wengi ambayo kwa sasa yako hatarini.

Ombi hili la Kardinali Sarr ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Magharibi, katika mkutano wake uliofanyika hivi karibuni huko Tambacounda, Senegal. Tarehe 23 Novemba 2014, Volkano ililipuka na kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao nchini Cape Verde. Zaidi ya watu 850 wamehamishwa kutoka kwenye makazi yao kwa kuhofia usalama wa maisha na mali zao.All the contents on this site are copyrighted ©.