Bwana Dragan Covic akutana na Papa Francisko mjini Vatican
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 15 Desemba 2014 amekutana na kuzungumza
na Bwana Dragan Covic, mwanachama kutoka Croatia katika jopo la Urais Bosnia na Erzegovina.
Viongozi hawa baadaye wamezungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa
Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti aliyekuwa Katibu mkuu
wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.
Viongozi
hawa wawili wamejadili kwa kina na mapana hali ya nchi hizi mbili na kwa namna ya
pekee mchango wa Kanisa Katoliki katika mchakato wa maendeleo endelevu ya ujenzi wa
nchi hii baada ya kukumbukwa na mafuriko mwaka 2013 yaliyosababisha hasara kubwa.
Wameridhika na mahusiano mazuri kati ya pande hizi mbili; mafanikio na changamoto
zilizopo katika utekelezaji wa Itifaki ya mwaka 2006, ambamo pamoja na mambo mengine
Serikali na Kanisa vilitiliana sahihi ya kushirikiana kwa karibu zaidi kwa ajili ya
mafao ya wengi. Mwishoni, viongozi hawa wamegusia masuala mbali mbali ya kikanda na
kimataifa.