2014-12-15 15:02:51

Balozi Savoie awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 15 Desemba 2014 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Dennis A. Savoie, Balozi mpya wa Canada mjini Vatican. Bwana Savoie alizaliwa kunako tarehe 9 Februari 1945, ana mke na watoto wawili. Kunako mwaka 1968 alihitimu masomo yake ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Moncton na kubahatika kufanya kazi mbali mbali nchini Canada.

Kuanzia Mwaka 1969 hadi mwaka 1996 amefanya kazi katika Kampunu ya Umeme ya New Brunswick Elecritic Power Corporation hata kufikia ngazi ya Makamu wa Rais wa Kampuni. Kunako mwaka 1996 alistaafu kutoka kazini na kuanza kujishughulisha na kazi za kujitolea pamoja na kuwa ni mshauri katika masuala hayo hadi mwaka 2000.

Kunako mwaka 2000 hadi mwaka 2004 alikuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Wauguzi cha Brunswick. Kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2006 alikuwa ni kaimu mtunza fedha wa Chama cha Kitume cha Colombo na kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2013 alichaguliwa kuwa ni Makamu mkuu wa Chama cha Kitume cha Colombo, huko Connectitus, Canada.All the contents on this site are copyrighted ©.