2014-12-13 10:38:29

Ujumbe wa Papa kwa Mkutano wa kutoa tuzo ya heshima ya amani 2014


Baba Mtakatifu Francisco siku ya Ijumaa alituma ujumbe wake kwa Washiriki wa Mkutano wa XIV , kwa ajili ya utoaji wa tuzo ya Amani ya mwaka 2014, kwa watu walioonekana kutenda vyema zaidi katika kutetea amani. Mkutano unaofanyika mjini Roma tangu Ijumaa 12-14 Desemba.

Ujumbe wa Papa ulio tumwa na Katibu wa Vatican , Kardinali Pietro Parolin kwa niaba ya Papa, umetaja hisia halisi zilizomo ndani ya moyo wa kila mtu, awe mwanaume au mwanamke kwamba wote wana hamu ya kuwa na maisha matulivu, maisha ya amani, ikiwa ni pamoja na ile hamu ya kujenga udugu usioweza tanguliwa, hamu ya udugu ambayo hutokana na uzuri wa kushirikiana na wengine, inayomwezesha mtu kuwaona wengine kama si maadui au wapinzani, lakini kama ndugu, kaka na dada, katika kuishi maisha ya kukubalika na kuvutiwa na wengine, kama ilivyoelezwa katika Ujumbe wa Siku ya Kuombea Amani Duniani kwa mwaka 2014.

Baba Mtakatifu amefurahia na kutoa heshima zake za dhati kwa washiriki wa mkutano huu, kwa ajili ya kazi yao ya kukuza amani na udugu kati ya watu , na kwa jitihada zao za kutoa majawabu yanayofaaa katika migogoro inayojitokeza katika maisha yetu ya kila siku.
Papa pia ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha Mkutano huu , kutoa heshima za kipekee, kwa Nelson Mandela, aliyeiachia dunia mfano wa kupata amani bila kutumia vurugu, ila kwa njia ya majadiliano na maridhiano . Papa ameomba urithi huu wa Mandela uendelee kuhamasisha ujenzi wa amani na mapatano duniani. Papa Francis anaomba kwamba, wote waweze sasa kuwa na moyo mpya katika kazi za kidharura za kurejesha amani, na kwamba kazi yao iweze kuleta mavuno tele duniani. Pia Papa aliwahakikishia sala zake ili kwamba maamuzi yawe yaweze timiza makusudi ya mkutano wao.
All the contents on this site are copyrighted ©.