2014-12-13 10:38:08

Siku kuu ya Mama yetu wa Guadalupe : ishara ya amani.


Katika adhimisho la Siku kuu ya Bikira Mama Yetu wa Guadalupe, aliyemtokea Mtakatifu Juan Diego , miaka 483 iliyopita, Maaskofu wa Mexico , wametoa mwaliko kwa waumini kuvaa vazi jeupe kama ishara ya kuzama katika sala za kuombea haki na amani kwa taifa lao la Mexico na kutolea sadaka ya Ibada ya Misa kwa nia hiyo.
Na pia kwa mwaka huu , umati mkubwa wa waamini uliandamana na kukusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Guadalupe, kutolea sala zao kwa Mama yetu wa Tepeyac , ambaye pia ni mlinzi wa taifa ya Mexico na Amerika ya Kusini yote.
Salaam na ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisco kwa ajili ya Siku Kuu hii, ulikazia zaidi maombi kwa ajili ya msamaha na baraka kwa watu wa Mexico na mataifa mengine na , na wakati huo huo, kutolea sifa na shukurani zenye kuonyesha utambuzi wa maana ya kiroho ya sherehe ya Ekaristi.
Papa amesema, Sikukuu hii ya Mama yetu ya Guadalupe, pia imemkumbusha pia ziara yake aliyoifanya Mexico, ambamo mama Bikira Maria alimsindikiza na huruma yake ya kimama, na hivyo wanaweza kuimba Utenzi Mkuu wa Mama Maria , na kuyaweka maisha yote katika dhamana yake maisha ya watu wa bara la Amerika ya Kusini na utume wa Kanisa.
Papa alieleza na kurejea tukio la Juan Diego kutokewa na Bikira Maria huko Tepeyac, Mama aliye jitambulisha kuwa ni Bikira kamili wa milele, Mama Maria, ilikuwa ni ishara kubwa, kama alivyotajwa katika kitabu cha ufunuo , ikaonekana mbinguni ... mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake" (Ufu 12,1), ambaye anakubali kuwa mfano wa jadi ya utamaduni i na kidini, na anayetangazwa na kutolewa kama dhabihu, Mwana wake wa pekee kwa ajili ya watu kufanywa wapya.
Baba Mtakatifu katika ujumbe wake anaendelea kutolea maombi kwa ajili ya Amerika ya Kusini , akiwa amejawa na matumaini makubwa juu ya bara hilo. Papa analitaja bara hili la Amerika Kusini kuwa bara la matumaini, ambalo mpaka sasa limeanza kuwa mfano wa maendeleo mapya, katika kuchanganya mila ya Kikristo na maendeleo ya kiraia, haki na usawa na maridhiano, maendeleo ya sayansi na teknolojia na hekima ya mwanadamu. Matunda ya mateso kuwa furaha na matumaini. Hata hivyo Papa ameonya kuwa inawezekana kuweka tumaini hili, kupitia uwepo mkubwa wa ukweli na upendo, msingi wa ukweli wote, injini ya halisi maisha mapinduzi mpya.

Papa aliiweka nia na hamu hii katika madhabahu kama zawadi ya kumpendeza Mungu. Hamu ya kupata msamaha wake na kuamini katika huruma yake, na kusherehekea sadaka na ushindi Pasaka ya Bwana wetu Yesu Kristo. Alisisitiza ,Yeye ni Bwana mkombozi wa hali zetu zote za wasiwasi , hofu na mateso, na yote yanayotokana na dhambi na utumwa. Anatuita kuishi maisha halisi, maisha zaidi ya kibinadamu, kuishi pamoja kama ndugu na wana, sasa kufungua milango ya "dunia mpya na mbingu mpya" (Ufu 21,1). Na sisi tunawasihi Bikira Maria, katika wito wake wa Guadalupe, Mama wa Mungu, Malkia na Mama yetu, Kigoli wetu na mdogo wetu , kama Mtakatifu Juan Diego, alivyoweza kumwita majina yote ya upendo na yenye kumkomaza katika ucha Mungu, na yanayo saidia kuendelea kuongozana naye na kutoa msaada wake na kulinda watu wote. Aidha hotuba ya Papa imeonyesha kutambua kwamba Mama Bikira Maria wa Guadalupe, huongoza kwa mkono wake, mahujaji wote wanaofanya hija katika madhabahu mbalimbali katika nchi hizi, wakitafuta kukutana na Mwana wake, Yesu Kristo, Bwana wetu, anayeishi katika Kanisa moja lake takatifu, ndani ya 'Ekaristi, na katika hazina ya ujumbe wake na mafundisho yake , kupitia katika watu takatifu, aminifu mwaminifu wa Mungu, na katika wale ambao wanateseka katika unyenyekevu wa moyo. Na iwe hivyo. Amina!








All the contents on this site are copyrighted ©.