Baba Mtakatifu Francisco siku ya Ijumaa alikutana na viongozi wa Jeshi la Wokovu mjini
Vatican. Katika hotuba yake , Papa alionyesha kufurahia na kutambua juhudi zao zinazojulikana
katika kazi za uinjilishaji na huduma za kitume. Na kwamba ziara yao, ni matunda
mazuri ya mawasiliano ya mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni, kati ya Jeshi
la Wokovu na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo, ikiwa ni pamoja
na mfululizo wa mazungumzo ya kiteolojia kwa lengo la kukuza uelewa mzuri kwa wengine,
kuheshimiana na kushirikiana mara kwa mara.
Papa ameonyesha imani yake kwamba
, Wakatoliki na Jeshi la Wokovu , wataweza kuendelea kutoa ushuhuda wao katika maisha
ya kawaida kwa Kristo na Injili, katika ulimwengu wa sasa wenye kuwa na hitaji kubwa
la kuiishi huruma ya Mungu isiyo kuwa na mipaka.
Papa aliendelea kusema,
Wakatoliki na Jeshi la wokovu, kwa pamoja na Wakristo wengine, wanatambua kwamba
wanahitaji wenye kuwa na kiu kwa Mungu, wana nafasi ya pekee katika moyo wa Mungu,
kwa kuwa Bwana Yesu Kristo mwenyewe alikuwa maskini kwa ajili yetu (cf. 2 Kor 8: 9).
Matokeo yake, Wakatoliki na Jeshi la Wokofu , mara nyingi hukutana katika maeneo
ya pembezoni mwa jamii. Na hivyo yanakuwa ni matumaini ya Papa Francisco kwamba,
imani ya pamoja katika Yesu Kristo Mwokozi, mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu
(cf. 1 Tim 2: 5), inakuwa milele, msingi imara wa urafiki na ushirikiano kati ya Wakatoliki
na Jeshi la Wokovu.
Aliendelea kusema, Kanisa ambalo hujitokeza mbele , ni
jumuiya ya mitume wamisionari, wanaochukua hatua ya kwanza mbele , wale wanaojihusisha
na kutoa mkono wa msaada , wenye kuzaa matunda na kufurahi. Ni jumuiya ya kueneza
injili, inayotambua kwamba , ni mpango wa Bwana, ndiye aliyetupenda kwanza (cf. 1
Jn 4:19), na kwa hivyo tunaweza kusonga mbele, kwa ujasiri, kuchukua hatua, kuwaendea
wengine, kuwatafuta wale waliokwisha kwenda mbali, kusimama katika njia panda, na
kuwakaribisha wakiwa. Jumuiya kama hiyo ina hamu isiyokuwa na mwisho inayopenda kuionyesha
huruma ya Mungu , na matunda ya uzoefu wake wa nguvu za Huruma ya Baba ya milele
"(Waraka wa Kipapa wa Kitume wa Injili ya Furaha 24).
Baba Mtakatifu Francisco
amewaambia viongozi wa Jeshi la Wokovu kwamba , anasali ili kwamba katika dunia ya
leo, wafuasi wote wa Kristo waweze kutoa mchango wao katika kishawishi na nguvu sawia
inayoonyeshwa na Jeshi la Wokovu katika utumishi wa kujitoa, wenye kupendwa sana.
Pamoja na sifa hiyo, Papa aliendelea kutaja tofauti kati ya Wakatoliki na Jeshi la
Wokovu kwamba ni hoja mbili za kiteolojia na kikanisa , tofauti hizo na visiwe vigezo
vya kuzorotesha ushuhuda wa upendo wa Mungu wa pamoja na upendo kwa jirani, upendo
ambayo una uweza wa kutoa msukumo kwa ahadi za pamoja ili kurejesha heshima ya
wale ambao wanaishi pembezoni mwa jamii .
Papa Francisco alikamilisha hotuba
yake na maneno kwamba , anatolea sala zake kwa Mungu kwa ajili ya kazi za Jeshi la
Wokovu. Na watu wengine walio katika hali ngumu waendelee kutegemea juhudi za Jeshi
la Wokovu , zinazoweza kuwaonyesha mwanga Kristo na kuangazia mahali pa giza katika
wa maisha yao. Papa amelitakia Jeshi la Wokovu kujazwa na zawadi ya Roho Mtakatifu
kwa hekima, ufahamu, ujasiri na amani, na hivyo kushuhudia Ufalme wa Bwana katika
mateso ya dunia hii. Na kwamba anahitaji maombezi yao.