2014-12-12 09:50:57

Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo:" Nipe Maji Ninywe "


Maaskofu Katoliki Kenya wametoa ujumbe wao kwa Wakristo wote , kwa ajili ya Wiki ya Sala ya kuombea Umoja wa Wakristo, ambalo kila mwaka inafanyika kuanzia tarehe 18-25 Januari. Kwa mwaka 2015, wiki hii, inaongozwa na kauli mbiu: “Nipe maji ninywe”(Yh4,7).
Mwenyekiti wa Tume ya Kiekumeni Kwa Baraza la Maaskofu Kenya, Askofu Peter Kairo, akitoa ujumbe kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Kenya anasema kwamba, Mada ya mwaka huu ambayo imeegemea katika aya za Yesu kukutana na mwanamke Msamaria kisimani, ni mwongozo katika juhudi zote za kiekumeni na himizo la kuishi kwa kutegemeana mmoja kwa mwingine licha ya kuwa tofauti. Ni wito wa kujenga umoja na mshikamano na udugu kati ya waamini.

Ujumbe unaendelea kueleza kuwa, aya hiyo ni wito wa kufanya upya dhamana katika kushirikiana. Ni mwaliko wa Bwana kutoa maji kwa watu wote wanao waendea kama wahitaji, wanaotaka kujua, kujadiliana na kukubaliana na kila mmoja kuishi utume wa Kanisa. Wakiwa na uthabiti katika kutegemea Bwana , upendo wake una uwezo wa kubadilisha yote , kama ilivyo kwa mtu mwenye kiu kunywa maji. Bwana ni chanzo cha maji hai yenye kuzaa matunda ya umoja halisi, ambayo Waamini wote wana kiu hiyo kwa muda mrefu.

Hivyo, Askofu Kairo, anakumbusha kuwa, mwaka huu, mwongozo katika tafakari za Wiki la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, umeandaliwa na Baraza la Kitaifa, linalounganisha Makanisa ya Kikristo ya Brazil, taifa lenye dini nyingi za Kikristo lenye kukabiliwa na "uso changamoto nyingi za kutovumiliana kati ya madhehebu, na lenye kuwa na kiwango cha juu cha ukatili dhidi ya wanawake na watu wa asilia.

Askofu Kairo anahisi waamini wa Kristo Brazil kama ilivyo pia katika mataifa mengine, katika wiki hili wazamishe tafakari za kina katika kiu hii ya kuwa na umoja katika tofauti, kwa ajili ya kuishi kwa uhuru kikamilifu. Kuondoa tabia za kutovumilia wengine badala yake iwe kuheshimu tofauti halali na kukuza mjadala kwa ajili ya mema ya kawaida.


Askofu Peter Kairo pia ameligeukia taifa lake la Kenya na kusema hakuna tofauti na Brazil. Wakristo Kenya pia wako mbele ya changamoto hii uwepo wa “Ukristo unao nadiwa na kufungamana na utafutaji wa fedha, ambao umeibua makundi ya ubabe, vurugu na ubabe usiokuwa na kiasi katika baadhi ya maeneo.
Hivyo, Ujumbe unakamilisha na wito kwamba, Wiki hili la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, ni nafasi ya kushuhudia matunda mazuri ya neema ya Mungu, katika kuwapokea na kuwakaribisha wengine kwa moyo mkunjufu licha ya kutofautiana, na kutokuwa wakamilifu,bado Roho Mtakatifu anasukuma waamini katika maridhiano na umoja ,“Nipe maji ninywe. “
All the contents on this site are copyrighted ©.