2014-12-12 07:40:17

Tatizo la ekolojia linagusa kanuni msingi za kimaadili


Majanga makubwa yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ya kimaadili inayohitaji mabadiliko makubwa ya kifikra, ili kuleta matokeo yanayofaa kwa kuwa na mwelekeo mpya wa maisha. Vigezo vinavyowasaidia walaji kuchagua na kuweka mitindo mipya katika maisha ni utafutaji wa ukweli, uzuri, wema na ushirikiano wa pamoja kwa ajili ya mafao ya wote. Mitindo ya maisha haina budi kuwa na kiasi, ukadiri na nidhamu.

Mwanadamu katika miaka ya hivi karibuni amekuwa ni chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira na matokeo yake yanahatarisha ekolojia nzima, changamoto na mwaliko kwa Jumuiya ya Kimataifa kushikamana kwa dhati katika mchakato unaopania kudhibiti majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi, ili kuendeleza kazi ya uumbaji, ambayo mwanadamu amekabidhiwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mafao yake kwa sasa na kwa kizazi kijacho.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitando ya kijamii anawakumbusha kwamba, ekolojia ni jambo muhimu sana katika maisha na ustawi wa binadamu na kwamba, linagusa kanuni maadili. Itakumbukwa kwamba, wafuasi wa Baba Mtakatifu kwenye akaunti yake ya twitter wamefikia millioni kumi na sita!.All the contents on this site are copyrighted ©.