2014-12-12 14:50:22

Kardinali Jorge Marìa Mejìa amezikwa Roma


Baba Mtakatifu Francisco , mapema Alhamisi , Kanisa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican, aliongoza Ibada ya Misa ya wafu kwa ajili ya kifo cha Kardinali Jorge Maria Mejia, Mkutubu Mstaafu, aliyefariki mjini Rome, siku ya Jumanne 9Desemba, akiwa na umri wa miaka 91. Na ibada ya Mazishi iliongozwa na Mkuu wa Dekania ya Makardinali, Kardinali Angelo Sodano, akishirikiana na umati wa Makadinali wapatao thelathini, akiwemo Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, pia Maaskofu wakuu wanne na kundi na Maaskofu.
Marehemu Kardinali Jorge Mar’a Mejìa, amezikwa katika kanisa lake la Mtakatifu Jerome wa Upendo , lililoko katika uwanja wa Farnese, jijini Roma. .

Kardinali Angelo Sodano, katika homilia yake , alisema , "kwa mpendwa wetu Kardinali Jorge Mejía, umefika wakati wake wa kurejea katika nyumba ya Baba, baada ya kuishi katika dunia hii, kwa uwepo mzuri wa umri wa miaka tisini, ambayo aliishi katika mwanga wa imani, kwanza katika nchi yake pendwa ya Argentina na baadaye hapa mjini Roma, katika huduma ya Kiti Kitakatifu. Aliteuliwa kuwa mtumishi katika Kiti Kitakatifu na Papa Paulo VI, mwaka 1977,kama Katibu wa Tume ya Mahusiano na Uyahudi.

Kardinali Sodano , aliendelea kueleza historia ya Marehemu Kardinali Jorge kwamba, daima alibeba ndani ya moyo wake kimyakimya urithi wa utamaduni kiteolojia , aliojipatia baada ya masomo yake huko Buenos Aires na kisha kukamilishwa hapa mjini Roma, katika Chuo ch Kipapa cha Angelicum na Taasisi ya Kipapa ya Biblia. Ni mtu aliyekuwa ameyatolea maisha yake kama mtaalam wakati wa mchakato wa Mtaguso Mkuu wa II, katika miaka ya 1963-1964, na baadaye mwaka 1977, aliletwa karibu na Makao Makuu ya Jimbo Takatifu , kwa ajili ya kutoa mchango wake wa thamani katika ofisi mbalimbali, kwanza kwa utawala wa Papa Paulo VI na kisha Papa Yohana Paul II, katika Baraza la Haki na Amani, katika Usharika kwa ajili ya Maaskofu na Maktaba Vatican.

Na hivi karibuni , alipatwa na maradhi yenye kuwa na maumivu makali, yaliyo rudisha nyuma , utendaji wake, na alitumia siku zake mwisho kwa utulivu mkubwa, akimwiga Musa, aliyewaambia wana wa Israel, wakati wakielekea nchi ya ahadi "kumtazama yeye asiyeonekana." Ilikuwa mtazamo huohuo pia ulio andikwa na Papa Paulo VI katika maandishi yake maarufu "Juu ya Wazo la kifo." "Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa ndugu yetu mpendwa Jorge, ambaye alitumia siku zake za mwisho kuombea uenezaji wa Ufalme wa Mungu.

Siku za hivi karibuni kabla ya kifo chake, Kardinali Sodano alikwenda mjulia hali na kumfariji, na maneno sisi sote tuko katika mikono ya Bwana , naye mgonjwa alifungua macho yake na kusema, tupo katika mikono mizuri . Kardinali Sodano , alisema, na hilo ndilo tumaini la kila Mkristo , kukamilisha safari ya maisha ya hapa duniani , kwa imani ya kwenda katika mikono ya Bwana. “Hii ni hekima ya Kikristo ambayo ili angazia njia ndefu ya ndugu yetu mpendwa Jorge. Na maisha yake yamebaki daima kuwa mfano wa kuishi katikati yetu, na kwa taifa lake pendwa la Argentina”. Tunamwobea pumziko la amani katika mikono ya Bwana aliyemtumikia.
All the contents on this site are copyrighted ©.