2014-12-11 07:25:09

Kanisa ni mama anayetambua utajiri na mapungufu yake!


Furaha ya kanisa ni kuwa mama, kwenda kuwatafuta kondoo waliopotea. Papa Francisko , alieleza Jumanne mapema wakati wa Ibada ya Misa, katika Kanisa la Mtakatifu Marta, mjini Vatican. Alisema Kanisa haliwezi kuwa mhudumu kamilifu iwapo litakuwa na woga na kujifungia na iwapo halitakuwa kama mama . Na hivyo , katika kuwa hivyo, mwaliko unatolewa kwa Wakristo kuwa na furaha kwa ukombozi wa huruma wa Yesu

Baba Mtakatifu Francisko, akilenga katika somo la kwanza ambamo Nabii Isaya anazungumzia dhiki za wana wa Israel baada ya Uhamisho wa Babeli , homilia yake ilihimiza waamini kufungua milango ya mioyo, kwa ukombozi wa Bwana. Watu - alisema – wana haja ya kufarijika na ukombozi. Na uwepo wa Bwana hufariji. Faraja ambayo pia inaonekana wakati wa dhiki. Lakini kwa bahati mbaya , Papa alionya, mara nyingi binadamu huikosa faraja hii kutokana na uhaba wa imani, daima hutafuta faraja katika mambo yake mwenyewe. , hata katika udhaifu wake na dhambi zake. Hiyo ndiyo asili ya ubinadamu wetu . Lakini kumbe , Papa alisisitiza , wakati Roho Mtakatifu anapokuja kutufariji , anatuletea hali nyingine ambayo hatuwezi kuidhibiti, ila inakuwa ni hali halisi, ya kujiweka katika ukombozi wa Bwana"

Na kwamba, faraja yenye nguvu zaidi ni huruma na msamaha. Papa alieleza kwa kuangalisha mawazo katika mwisho wa sura ya kumi na sita ya Kitabu cha Nabii Ezekiel, ambamo mnazungumzia orodha ya dhambi kwa watu wengi na kujisalimisha na ulipizaji wa kisasi , faraja na msamaha
Tafakari ya Papa iliendelea kutazama ni ipi faraja inayopatikana katika kanisa. Na kwa jinsi gani na lini Kanisa hufurahi apale mtu anapoisikia kufarijiwa na huruma ya Mungu na Msamaha wa Bwana , akisema kuwa ni pale mtu anapoacha kujifungia ndani mwake mwenyewe.Ile furaha ya kutoka nje kwenda kuwatafuta ndugu wengine wake kwa waume waliopotea , wale waliokwenda kwenda mbali na kanisa .hiyo ndiyo furaha ya kanisa .Hapo Kanisa linakuwa kama Mama , linakuwa kanisa hal lenye kuzaa matunda.
Papa alieleza na kukemea tabia ya kanisa kujifungia lenyewe, pengine kwa nia za kulinda taratibu zake au utendaji kamilifu, au katika kutunza nafasi yake , kuwa safi , lakinikw kufanya hivyo hukosa furaha , hukusa sherehe hukosa amani , na kuwa kanisa lisilo na imani, lenye wasiwasi na , huzuni, kanisa ambayo ina zaidi ya mjane mgumba, kanisa kama hilo halihudumu lakini yanakuwa ni makumbusho kanisa. Furaha ya Kanisa kuzaa matunda, furaha ya Kanisa ni kwenda nje lenyewe kutoa maisha, furaha ya Kanisa ni kwenda kuangalia wale kondoo waliopotea, furaha ya Kanisa ni hasa imo katika huruma ya mchungaji, huruma ya Mama Kanisa.

Mwisho Papa alirejea tena kifungu kutoka Isaya, akielezea, kuyachukua maneno hayo , kama mchungaji anayechunga kundi l wanakondoo wake kwa mikono yake mwenyewe . Hiyo ndiyo furaha ya Kanisa kutoka nje ya lenyewe na kuzaa matunda.
Papa alikamilisha kwa kutolea sala akisema, "Bwana atupatie neema ya kazi, kuwa Wakristo wenye furaha katika kuzalisha matunda, na aliomba ulinzi wa Mama Kanisa, uwalinde wana wake dhidi ya kuanguka katika huzuni, hofu, tamaa na , wasiwasi nakatika kuwa kamilifu kwenye huduma zake lakini hawana wazao. . Bwana utufariji na ukombozi wa mama kanisa utuwezeshe kutoka nje ili wote wapate kufarijika na ukombozi wa huruma ya Yesu na huruma katika msamaha wa dhambi zetu.
All the contents on this site are copyrighted ©.