2014-12-10 15:55:58

Kardinali Giorgio Jaime Mejìa


Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Alejandro Jaime Mejia, kilichotokea usiku wa Jumatatu kuamkia siku ya Jumanne wiki hii. Kardinali Mejìa amefariki akiwa na umri wa miaka 91, baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu. Baba Mtakatifu Francisco, Novemba 16, alikwenda kumjulia hali.

Kufuatia kifo hicho, Papa akiwa ameshikwa na simanzi, alipeleka kwa njia ya telegramu, salaam zake za rambirambi kwa kaka wa Marehemu , ambamo alisema katika maombi yake atamkumbuka kumwombea Marehemu ambaye kwa muda wa miaka mingi wamekuwa marafiki.

Salaam hizi zinaendelea kumwombea Marehemu, ili kwamba , mwanga wa fumbo la Pasaka la Bwana Mfufuka, liweze kuangazia njia na kujaza matumaini katika njia ya maisha ya Kikristo, na kumbukumbu ya sadaka ya maisha ya katika kazi za Uinjilishaji za Marehemu. Papa pia amewaombea faraja za Bwana wote walioguswa na msiba huu , na kuwatakia baraka na faraja zake za kitume.

Ibada ya Misa ya wafu kwa ajili yake itafanyika Alhamisi 11 Desemba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa VaticanAll the contents on this site are copyrighted ©.