2014-12-09 15:22:16

Mwanadamu daima anahitaji wokovu


Kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku kuu ya Maria kukingiwa dhambi ya asili, Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, aliongoza Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis la Assisi. Katika homilia yake alisema, kusherehekea sikukuu hii ya Maria kukingiwa dhambi ya asili tangu alipotungwa mimba, katika Kanisa Kuu hilo, ambalo linahifadhi masalia ya watumishi wa Mungu wazawa maskini wa Assisi lakini ambao kwa sasa wamekuwa nuru kwa watu wengine, wanaotolea maombi yao kwao, ili kwamba vizazi vingi viweze kuona chanzo cha shangwe na sababu ya kutoa shukrani kwa Bwana, Yesu Kristo, Mkombozi wa dunia.

Kardinali Parolin aliongeza kuomba ili kwamba, sifa hii na shukrani zao, pia ziweze kubadilika na kuwa wakati wa furaha kuu, hasa wanapoelekeza pia mawazo yao kwa Bikira Maria, kumshukuru kwa "ndiyo", ndiyo iliyowezesha kumwingiza mwanae ulimwenguni , Mwana pekee wa Mungu, Yesu Kristo, Bwana na mkombozi wetu.
Kardinali aliendelea kutazama masomo yaliyosomwa katika liturujia ya Neno, kati ya mengine akionyesha mshangao wake kwa 'mwanamke kijana wa Nazareti, anaye ruhusu Mungu kukamilisha mpango wake wa wokovu na amani. Mwanamke anayekuwa chanzo cha furaha ya imani yetu, ambaye anaonyesha jinsi unyenyekevu unavyoweza kushinda kiburi na kuruhusu hata mtu mnyonge wa kijiji , kuwa Mama wa Mungu, katika historia ya wokovu na katika nafsi za waamini.

Na kwa masomo ya siku , waamini wanajifunza kwamba, mwanadamu daima anahitaji wokovu , na Mungu anaingilia kati, tena bila kudai malipo, anayayeyusha mawimbi yote ya ubaya, kama aya kutoka kitabu cha Mwanzo , zinavyosema, Mungu, alimwita adamu , Adamu uko wapi? Swali hili ni la muhimu na la kudumu kwa watu wote. Kama ilivyokuwa kwa Adam ni mtu wa kwanza, ndivyo ilivyo kwa binadamu wa leo, anayejaribu kujificha mbele ya macho ya Mungu, wakati anapo poteza nafsi yake, kupoteza uwezo wa kutambua sura na mfano wa Mungu na hivyo kupoteza haki kutembea katika mwelekeo sahihi.

Kardinali ameendelea kutazama hali halisi za wakati wetu , ambamo sayansi na teknolojia vimefanya maendeleo makubwa katika maisha ya binadamu, lakini mafanikio hayo yanayotishia hadhi ya mtu, yanahitaji kuongozana na uhakika wa maadili.

Na hivyo Sikukuu ya Maria kuzaliwa bila dhambi ya asili, inaangazia ubinadamu wetu na ndani ya Neno la Mungu mnaonekana sura mbili, katika sadaka ya matukio mawili ya maamuzi katika historia ya ubinadamu, mmoja kutoka kitabu cha Mwanzo na pili ni kutoka katika Injili.

Kardinali Parolin aliendelea kuelekeza mawazo kwa Mtakatifu Francis akisema , ni jambo jema kusikiliza maneno ya Mtakatifu Francis, anaposema, kumfuata Yesu maana yake ni kumweka Yesu katika nafasi ya kwanza kwa mambo yote. . Ni kuyavua mambo yote yanayoisonga roho, kujikana wenyewe, kuchukua msalaba na kuubeba ni pamoja na Yesu. Ni kuvua kila aina ya kiburi cha majivuno na kuachana na hamu ya kujikusanyia fedha na utajiri, miungu wa ulivyo navyo.

Na mwisho , aliwataka wote waliokuwa wakimsikiliza , kuutazama mfano wa maisha ya Mtakatifu Francis, ambaye alivivua vyote alivyokuwa navyo na kubaki mtupu. Aliyavaa maisha ya Kristo, bila kujibakiza. Na tuelekeze maombi yetu kwake yeye ambaye miaka sabini na mitano iliyopita alitangazwa Mtakatifu mlinzi wa Italia, atuombee pia sisi kujaliwa neema hii ya kutambua makosa yetu na kuachana nayo.

Pia alitolea Maombi kwa Mama Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, asaidie wafuasi wa mwanae, kupata ujasiri,wa kusonga mbele katika njia ya kumfuata Kristo. Waamini tuna haja ya kupata siri ya kufanywa upya na kupata ahueni, si tu kiuchumi na kijamii tu, lakini juu ya yote kimaadili na kiroho.
Mama Bikira Mkingiwa dhambi ya asili , utuhifadhi dhidi ya dhambi zote na kulinda sisi, utuonyeshe njia ya kupata nguvu ya kuendelea kutembea katika njia inayoelekea uzima wa milele.All the contents on this site are copyrighted ©.