2014-12-09 10:01:27

Askofu Vieira Dias ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Luanda, Angola!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Filomeno do Nascimento Vieira Dias, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Luanda, Angola. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Filomeno do Nascimento Vieira Dias alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Cabinda, Angola.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Dias alizaliwa tarehe 18 Aprili 1958. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 30 Oktoba 1983. Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu ya Luanda, Angola, tarehe 4 Oktoba 2003 na tarehe 11 Januari 2004 akawekwa wakfu kuwa Askofu. Tarehe 11 Februari 2005 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kabinda.

Na hatimaye, tarehe 8 Desemba 2014, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Filomeno do Nascimento Vieira Dias kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Luanda, Angola.All the contents on this site are copyrighted ©.