2014-12-09 12:01:58

Askofu Martin Musonde Kivuva ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mombasa, Kenya


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Martin Musonde Kivuva kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mombasa, Kenya. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Machakos, nchini Kenya.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Musonde alizaliwa kunako tarehe 10 Februari 1952 huko Muthetheni. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapdrishwa kunako tarehe 9 Desemba 1978, kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Mombasa. Kunako tarehe 15 Machi 2003 aliteuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Machakosi na kuwekwa wakfu hapo tarehe 3 Juni 2003.All the contents on this site are copyrighted ©.