2014-12-08 16:22:27

Tumwachie Mungu atufanye kuwa zawadi kwa ajili ya wengine


Kama Bikira Maria, Wakristo wote waweze kuwa na uelewa wa kujitoa sadaka kwa Mungu , kusema, "ndiyo" katika mapenzi yake na majitoleo kwa ajili ya kuhudumia wengine, kuwa "vyombo vya faraja, maridhiano na msamaha. Yalikuwa ni mawaidha na Matumaini ya Papa Francisko , wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, aliyoyatoa kwa kundi kubwa la mahujaji na wageni waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro , Jumatatu hii, ambayo ni Siku Kuu ya Maria kukingwa dhambi ya asili, tangu alipotungwa mimba.

Papa katika ujumbe wake alisema, Mjumbe wa Mungu anakuja na habari ya kushangaza zaidi ambayo haijawahi kusemwa na binadamu yeyote. . Utakuwa Mama wa Mwana wa Mungu. Na jibu linalotoka kwa Mama huyo , linakuwa jibu msingi la wateule wote na katika kila mfumo wa maisha ya Mkristo: Na iwe kwangu kama Mungu anavyonena. Papa Francisko, alilenga habari hii ya kutangazwa kwa Neno kuwa mwili, neno la kushangaza, ambamo ndilo msingi wa Siku Kuu ya Maria asiyekuwa na dhambi ya asili , ambamo tunapata tena hamu ya kutafakari upya nguvu za Maria, kutoa jibu kwa mapenzi ya Mungu. Mary analipokea neno akiwa imara lakini kwa unyenyekevu, kama inavyosomeka , ndiyo, na iwe kama ulivyosema. Maria alisema kwa unyenyekevu na iwe hivyo kama ulivyosema.

Na ndivyo pia sisi sote Mungu leo hii anatupa ujumbe wake na kusikiliza jibu letu, iwapo pia sisi tunajibu kwa unyenyekevu, na iwe kwangu kama ulivyosema. Kwa mujibu wa Mantiki ya Injili, hakuna jambo au manufaa, zaidi ya kusikiliza na kulikaribisha Neno la Bwana! Neno lililoandikwa katika Injili, au kutoka katika Biblia, ambamo Bwana husema nasi milele! Tunamtazama Maria wa Nazareti akituonyesha kwanza ubinadamu halafu kitendo, na kwamba ni lazima kumwachia Mungu katika kufanya kile anachotaka sisi tufanye. Ni Yeye Mungu anayetenda mengi ya ajabu. Maria alitunga mimba kwa imani. Neno hili la ajabu na siri hii ya kukubali neema ya Mungu, Maria, alipata upendeleo wa kipekee wa kuwa Mtakatifu aliyezaliwa bila kikwazo cha dhambi, unakuwa ni faraja na matumaini kwetu sote kwamba kwa kupitia Mwanae Yesu Kristo , pia sote tuna takatifushwa.

Papa aliendelea kusema, hata sisi, pia tunapewa neema na heri hii ya kupendwa na kuchaguliwa kabla dunia haijaumbwa, , ili tuwe watakatifu na bila mawaa. Maria alikuwa Mtumishi wa Mungu wa kwanza kupokea Neno la Mungu kwa ajili ya wokovu wetu, Neno tunalolipokea pia sisi kwa njia ya ubatizo na imani. Wote, hivyo, sisi na Yeye kupitia Yesu Kristo, tunasifu utukufu wa neema yake, neema ya isiyokuwa na ndoa, ambayo humiminwa kwetu katika ukamilifu wake.
All the contents on this site are copyrighted ©.