Jumapili Baba Mtakatifu akihutubia mahujaji na wageni wapatao 50 elfu waliotoka pande
mbalimbali za dunia, alikumbusha kwamba, Jumapili ya pili ya majilio, unaendelea
kuwa wakati wa maajabu ya kushangaza, yenye kutuhamasisha na kutoa mwamko mpya katika
matumaini ya kurudi kwa Kristo na kumbukumbu ya kuja kwake kihistoria.
Papa
alieleza huku akilenga katika liturujia ya Neno kwa Siku hiyo, kwamba, mna ujumbe
kwetu sote, ujumbe wa matumaini. Na alifanya rejea kutoka kitabu cha Isaya, aya zilizo
zungumzia "Faraja , kwamba Mungu atawafariji watu wake. Papa alifafanua kwa kifupi
juu ya aya hizo akisema zinahusu wakati wa furaha ya kukombolewa na wokovu, na wakati
wa kutazama kwa matumaini siku za mbele kwa kujiamini
Papa alieleza na kusema,
Isaya anarejea watu ambao walipita katika kipindi cha giza , lakini kwa sasa kwao
wakati wa kufarijika umewadia, ambamo huzuni na hofu imegeuka kuwa furaha, kwa sababu
Bwana mwenyewe anawaongoza watu wake katika njia ya ukombozi na wokovu.
Lakini,
Papa pia alisisitiza na kuonya , haiwezekani mtu kuwa mjumbe wa faraja ya Mungu kama
yeye mwenyewe hana uzoefu huo wa kuisha kwa kufarijiwa na kupendwa naye. Na ndivyo
ilivyo elezwa katika somo la Injili, kwamba watu wanapaswa kulibeba neno la Mungu
katika mikoba yao.Ujumbe wa faraja kutoka Somo la Isaya , unasikika tena Siku ya Jumapili
hii ya pili ya Majilio, ni mafuta yenye kupoza uchungu katika vidonda vyetu wa kiroho,
na kutupa motisha ya kufanya kwa bidii zaidi, katika kuiandaa njia ya Bwana. Papa
ametaja hali nyingi, zinazoweza onyesha faraja hii, lakini inahitaji kuwa ni ushuhuda
wa kweli wa maisha ya muumini yenye kuishuhudia faraja hii, hasa kwa wale walioonewa
na mateso, dhuluma na ukandamizaji, kuhusu wale ambao ni watumwa wa fedha, nguvu,
mafanikio, na kuipenda dunia. Sisi wote tumeitwa kuwafariji ndugu zetu, kushuhudia
kwamba Mungu tu anaweza kuondoa sababu za matukio ya kusikitisha katika yote kimwili
na kiroho pia. Papa alisema kwamba, ujumbe wa Nabii Isaya, unaendelea kuzungumza
ndani ya mioyo yetu hata leo, kutuambia kwamba Mungu husamehe dhambi zetu na kutufariji
kama sisi wenyewe tutamwendea kwa unyenyekevu na moyo wa majuto. Mungu, alisema
Papa Francisko, amekwisha angusha chini kuta za uovu na kujaza mashimo ya uovu wetu,
na kusawazisha matuta ya viburi na ubatili, na kusafisha njia ili tuweze kukutana
pamoja naye, iwapo tutaridhia.