2014-12-08 11:25:06

Jifunzeni kutoka kwa B. Maria ujasiri wa kumwilisha Neno la Mungu!


Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican wanasema kwamba, kwa kusoma na kujifunza Vitabu Vitakatifu, Neno la Bwana linaendelea kutukuzwa na hazina ya ufunuo ambayo Mama Kanisa amekabidhiwa ijaze zaidi na zaidi mioyo ya waamini, hasa pale wanaposhiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu, ili kukuza maisha ya Kanisa pamoja na kuheshimu zaidi Neno la Mungu linalodumu milele.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, tarehe 8 Desemba 2014, Mama Kanisa anapoadhimisha Sherehe ya Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili, anawaalika waamini kujifunza kutoka kwa Bikira Maria kuwa na ujasiri katika mchakato wa kulimwilisha Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha ya kila siku.All the contents on this site are copyrighted ©.