Salam za rambi rambi kufuatia kifo cha Malkia Fabiola
Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa Filippo, Mfalme wa Ubelgiji
na wananchi wake, kufuatia kifo cha Malkia Fabiola, aliyefariki dunia Ijumaa, tarehe
5 Desemba 2014 akiwa na umri wa miaka 86. Baba Mtakatifu anaiombea roho ya Marehemu
Malkia Fabiola, ipumzike kwa amani katika mwanga wa Ufalme wa Mungu.
Baba
Mtakatifu anawahakikishia wale wote walioguswa na msiba huu, uwepo wake wa karibu
kwa njia ya sala, ili waweze kuwa na matumaini katika maisha ya uzima wa milele.