2014-12-05 12:11:53

Mh. Padre Joseph Obanyi Sagwe ateuliwa na Papa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kakamega, Kenya!


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililotolewa na Askofu Philip Sulumeti wa Jimbo Katoliki Kakamega kung'atuka kutoka madarakani kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401ยง Ibara ya 1 na hapo hapo ameteua Mheshimiwa Padre Joseph Obanyi Sagwe, Paroko wa Kanisa kuu na Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Kisii, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kakamega, nchini Kenya.

Askofu mteule Joseph Obanyi Sagwe alizaliwa kunako mwaka 1967 huko Kebiro, Jimbo Katoliki la Kisii, Kenya. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrsihwa tarahe 25 Oktoba 1996. Baada ya Upadrisho alitekeleza utume wake kama Paroko msaidizi na Mratibu wa shughuli za kichungaji Jimboni Kisii kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 1999.

Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2004, alijiendeleza kwa masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterani kilichoko mjini Roma. Aliporejea Jimboni mwake kunako mwaka 2004 aliteuliwa kuwa Paroko wa Kanisa kuu la Jimbo Katoliki Kisii na kuanzia Mwaka 2005 alikuwa ni Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Kisii, ambalo liko chini ya Jimbo kuu la Kisumu, Kenya.All the contents on this site are copyrighted ©.