Tanzania yapata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Saudia!
Serikali ya Tanzania imewekeana sahihi mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi
ya shilingi bilioni 45.2 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha
miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani
Zanzibar. Mkataba huo umesainiwa Alhamisi, tarehe 4 Desemba 2014 Jijini Dar es salaam
na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi
wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
Akiongea na waandishi
wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada amesema kuwa kati ya mkopo huo shilingi
bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa
maji katika wilaya za Same na Mwanga na shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi
wa barabara Pemba, visiwani Zanzibar.
Waziri Saada alilishukuru Shirika la
Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua
tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa
vya Pemba. Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni
110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine
wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.
Mradi wa maji wa Same -
Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini
amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji
nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao
kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi
kutafuta maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia
Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi
Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika
kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo. Hafla
hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na
wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.