2014-12-04 08:47:30

Mshikamano wa upendo na wananchi wa Karamoja, Uganda


Imekwishagota takribani miaka 20 tangu alipofariki dunia Padre Vittorio Pastori, aliyefahamika na wengi kama "Don Vittorione". Ni kiongozi aliyejitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wa Karamoja, walioko nchini Uganda.

Mara baada ya Katekesi, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 3 Desemba 2014 alipatiwa zawadi na Chama cha Kitume cha Ushirikiano na Maendeleo Barani Afrika, kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kitakachotumiwa na wananchi wa Karamoja, walioko nchini Uganda. Chama hiki katika utume na maisha yake kwa kipindi cha miaka arobaini na tatu iliyopita, kimeweza kuchimba visima vya maji elfu moja kwa ajili ya matumizi ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo la Karamoja, nchini Uganda.

Katika tukio hili, Baba Mtakatifu amemkumbuka Padre Vittorione kwa ushuhuda wake katika azma ya Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.All the contents on this site are copyrighted ©.