Majadiliano ya kidini yanapania kujenga na kudumisha amani!
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano asubuhi tarehe 3 Desemba 2014 amekutana na kuzungumza
na viongozi wa dini ya Kiislam na Kikristo wanaofanya mkutano wao mjini Vatican chini
ya uongozi wa Kardinali Jean Louis Tauran, Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano
ya kidini. Baba Mtakatifu amewashukuru na kuwapongeza kwa kumtembelea, jambo muhimu
sana katika kukuza na kudumisha udugu kati ya watu!
Baba Mtakatifu anawapongeza
kwa kazi na utume wao, katika mchakato unaopania kuwasaidia waamini wa dini hizi mbili
kufahamiana vyema zaidi, ili kudumisha amani na utulivu. Baba Mtakatifu anasema, hii
ndiyo njia ya amani inayojikita katika majadiliano ya kidini yanayosimikwa katika
uhalisia wa maisha ya watu katika umoja, upendo na mshikamano wa dhati.