Taarifa ya Shirika la Afya Duniani, inaonesha kwamba, hadi kufikia tarehe 29 Novemba
2014, watu waliofariki kwa ugonjwa wa Ebola wamefikia 7, 000, wengi wao wakiwa ni
wale wanaotoka katika nchi za Afrika Magharibi. Hadi sasa WHO haijatoa maelezo ya
kina kuhusiana na kuongezeka kwa idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa
Ebola.
Zaidi ya watu 16, 000 wamepimwa na kukutwa wakiwa wameambukizwa virusi
vya ugonjwa wa Ebola, tangu ulipofumuka huko Guinea, mwezi Machi, 2014. Guinea, Sierra
Leone na Liberia ndizo nchi ambazo kwa sasa zimeathirika kwa kiasi kikubwa kutokana
na kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.