Papa Francisko asema ziara yake Uturuki ni neema katika majadiliano ya kiekumene
Baba Mtakatifu Francisko, katika siku ya tatu na ya mwisho, ya ziara yake Uturuki,
kati ya mengine, alishiriki katika katika Ibada Takatifu iliyofanyika ndani ya Kanisa
Kuu la Kiekumeni la mjini Istanbul, kwa ajili ya Maadhimsho ya Siku Kuu ya Mtaktifu
Andrea, kwa mujibu wa Liturujia ya Kanisa la Kiotodosi. Sikukuu ya Mtakatifu Andrea
huheshimiwa kama mwanzilishi wa Kanisa katika Kiotodosi duniani. Liturujia ya kanisa
hili ni ya zamani.
Papa Francisko, akihutubia kwenye Ibada hii alimshukuru
Mungu kwa neema hii iliyomkutanisha na kiongozi wa kanisa la Kiotodosi, na kukutana
kwao uso kwa uso, kubadilishana mawazo kukumbatia kwa amani, na kuomba kwa ajili
ya umoja ni hatua muhimu katika safari ya kanisa, kurejesha usharika kamili wa wafuasi
wa Kristo. Na kwamba taratibu zote hizi , daima zinapaswa kuambatana na mazungumzo
ya kiteolojia. Mazungumzo halisi ya kina, si kukutanisha mawazo tu lakini kutazama
katika ukweli wa Injili.
Baba Mtakatifu ameendelea kusema kwamba, amekutana
na Kiongozi wa Kanisa la Kiotodosi kwa njia hii ya maridhiano na amani kati ya Wakatoliki
na Orthodox , si kama ni jambo alilolizua tu kujuuju lakini msingi wake ni hamu ya
tangu miaka hamsini iliyopita, waliyokuwa nayo watangulizi wao, Patriaki wa Kiekumeni
Athenagoras na Papa Paulo VI, waliopokutana miaka hamsini iliyopita Yerusalemu. Na
kwa furaha, ziara yake imekwenda sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kupita miaka
hamsini tangu azimio la Umoja wa Wakristo” Unitatis Redintegratio,”kupitishwa katika
Maazimio ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, juu ya Umoja wa Kikristo. Hati hiyo
ni msingi uliofungua njia mpya kwa ajili ya makutano ya Wakatoliki na ndugu zao wa
Makanisa mengine na jumuiya za kikanisa. Papa pamoja na kuzungumzia umoja wa Wakristo,
pia alirejea katika hali za maisha ya kawaida ndani ya jamii, akionyesha kujali kilio
cha watu wengi, wanaougumia kwa matatizo ya ukosefu wa mahitaji msingi si vitu tu
lakini pia ukosefu wa usawa na uganadmizwaji wa haki zao msingi. Papa amesema, Kanisa
haliwezi kupuuza juhudi za pamoja za kutoa utambulisho a nguvu kama wafuasi wa Bwana
mmoja Yesu Kristo, katika kuwahudumia wahitaji na wanyonge. Watu maskini wanaopaza
sauti wakiombe msaada. Sauti za watu maskini wake kwa waume, ambao ni wengi mno.
Wale wanaokabiliwa na utapiamlo mkali, kuongezeka ukosefu wa ajira, kuongezeka kwa
idadi ya vijana wasio na ajira, na kuongeza kutengwa na jamii.
Papa ametahadharisha
kwamba, matatizo haya yanaweza kuwa kati ya sababu kubwa za kuongezeka kwa matendo
ya kigaidi na uhalifu mwingine. Kanisa haliwezi kujificha au kuwa tofauti na kilio
cha ndugu hawa, Hatuna jingine Kanisa linaloweza kufanya zaidi ya kuhimiza nyezo
ya uadilifu, upendo na fadhila, kama silaha kuu katika kufanikisha mazingira ya kuokoa
wengi - lakini juu ya yote, msaada wa kutetea hadhi yao kama binadamu, ili waweze
kupata nguvu ya kiroho, na kwa mara nyingine, watu hao waone kuwa wao pia ni wahusika
wakuu wa maisha yao wenyewe.
Papa aliendelea kuzungumzia jinsi ya kupambana
na hali hizo katika mwanga wa Injili, hasa katika kuona sababu za miundo inayoleta
umaskini, na ukosefu wa usawa, uhaba wa kazi ya heshima na makazi, na kunyimwa haki
zao kama wanachama wa jamii na kama wafanyakazi. Amesema, Wakristo tumeitwa pamoja
kuondokana na utandawazi wa kutojali wengine. Huu ni wakati wa kujenga kujenga
ustaarabu mpya wa upendo na mshikamano.
Papa ametaja waathirika wa migogoro
katika sehemu nyingi za dunia, inayosikika, akirejea kilicho tokea Ijumaa katika
Msikiti wa Kano, Nigeria ambako watu zaidi ya mia wamepoteza maisha katika shambulio
la kigaidi lisilokuwa na maana. Papaanasema matendo kama haya hayawezi kukubalika
hasa pale mauaji yanayo fanywa kwa watu dhaifu na wasioweza kujitetea. Ameitaja kuwa
ni dhambi na inaonyesha kiburi dhidi ya Mungu. Matendo kama haya, ni dharau kwa
utu na heshima ya mtu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Papa alikamilisha
maelezo yake kwa kurejea tena katika njia ya kutembea kwa umoja na mshikamano , akiomba
Msaada wa Mtume Petro na Andrea nduguye kama walivyoomba watangulizi wa makanisa haya
mawili, waanzilishi wa Makanisa ya Constantinople na Kanisa la Roma. "Tunaomba Mungu
kwa ajili ya zawadi kubwa ya umoja kamili, na uwezo wa kukubali amani na utulivu
katika maisha yetu. Hebu kamwe tusisahau kuomba kwa ajili ya mtu mwingine".