Papa Francisko Kiongoza wa Kanisa Katoliki la Ulimwengu na Patriaki Bartholomew I,
Kiongozi wa kiroho wa dunia ya Waothodosi, Jumapili hii, 30 Novemba, nyakati za mchana,
waliweka sahihi zao katika hati ya Azimio la Pamoja kuonyesha hamu yao, katika kushinda
na kuondokana na vikwazo, vinavyotenganisha Makanisa yao mawili. Aidha katika tamko
hili, Viongozi hao wawili pia, wamelalamikia hali mbaya inayowakabili Wakristo na
wote wanaoteseka kwa sababu ya imani au itikadi yao katika kanda ya Mashariki ya
Kati. Azimio la viongozi hawa, linaihimiza jumuiya ya kimataifa kutoa hasa jibu sahihi,
kwa ajili ya kikomesha mateso na mahangaiko ya watu yanayosababisha na binadamu
Maelezo yao yameonyesha kujali hali zinazoendelea sasa Iraq, Syria na Mashariki
ya Kati. Kwa pamoja wanapenda kuona amani na utulivu vinarejeshwa katika mkoa huo
na watu kuwa na mapenzi ya kukuza utatuzi wa migogoro kwa njia ya mazungumzo na maridhiano.
Na pia wameonyesha kutambua na kushukuru juhudi zinafanyika katika kutoa msaada
kwa kanda hii , na wakati huo huo, kutoa wito wao kwa wanaohusika wote, kubeba
jukumu kwa ajili ya hatima ya watu, waweze kuimarisha dhamira yao juu ya jamii inayoteseka,
na kuwawezesha, wanaoteswa kwa sababu ya imani yao kwa Kristo, hasa wale wote, walioamua
kubaki katika nchi yao ya asili.
Tamko linasema , hawawezi kukata tamaa au
kujiuzulu katika kuwatetea Wakristo wa Mashariki ya Kati ambao wamekiri jina la Yesu
kwa kipindi cha miaka elfu mbili. Wengi wa ndugu hawa sasa wanateswa kulazimishwa
kwa ukali kutoka makazi yao. Mahali ambapo hata thamani ya maisha ya binadamu inapuuzwa
na kupotezwa bure. Hali hii inasikitisha hasa kwa wengi kutojali hali hiyo.
Tamko
linaendelea kueleza kuwa , changamoto zinazokabili dunia katika hali ya sasa zinahitaji
mshikamano wa watu wote wenye mapenzi mema. Kuona umuhimu wa kukuza mjadala wa kujenga
umoja, kati ya Ukristo na Uislamu kwa misingi ya kuheshimiana na urafiki. Waislamu
na Wakristo wameitwa kufanya kazi pamoja kwa ajili ya haki, amani na heshima kwa utu
na haki za kila mtu, hasa Wale katika mikoa ambako waliwahi kuishi kwa karne nyingi
katika mshikamano amani, lakini sasa na sasa wanapambana na maisha ya mateso na vita.
Kama viongozi wa Kikristo, wanatoa wito kwa viongozi wa dini zote, wajenge hamu ya
kuimarisha mazungumzo kati ya dini, kufanya kila juhudi kujenga utamaduni wa amani
na mshikamano kati ya waaamini na kati ya watu.
Azimio hilo limefungwa
na ombi "Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na katika kila njia.
Bwana na awe pamoja nanyi nyote "(2 Thes 3:16).