2014-11-30 12:18:24

Papa ashiriki sala ya kiekumene na Patriaki Bartolomeo wa kwanza!

Jumamosi majira la jioni , Papa Francisko alishiriki katika sala ya Kiekumeni kama ilivyoandaliwa na Patriaki Bartholomew I, Mkuu wa Kanisa la Kiotodosi la Constatinopol . Sala hiyo ilifanyika katika Kanisa Kuu la Kipatriaki la Mtakatifu George la Phanar.
Ibada hii ilipambwa kwa nyimbo wakati Papa na Patriaki walipoingia ndani ya Kanisa, ikifuatiwa na sala za masifu na shukurani kwa Mungu, pia yalitolewa maombi kuwaombea viongozi wa Kanisa ,Papa na Patriaki na kwa ajili ya Umoja wa Makanisa ya Mungu. Neno la Mungu lililosomwa kutoka Kitabu cha Nabii Zakaria 8, 7-17( “ Bwana Mungu wa Majeshi asema, Tazama , nitawaokoa watu wangu kutoka nchi ya Mashariki na toka Magharibi , nao nitawaleta ....”).
Baba Mtakatifu katika homilia yake, alirejea aya za Neno la Mungu kutoka Kitabu cha Nabii Zakaria , na kuomba neema ya Bwana iweze kuleta upya na kuwadumisha katika misingi ya kutembea pamoja siku hadi siku , wakiwa wameimarika katika mwamba wa furaha na matumaini. Msingi huo ni ahadi ya Bwana .
Papa alionyesha shukurani zake zao dhati kwa ndugu yake katika Bwana Bartholomew 1, kwa mapokezi na makaribisho mazuri yenye kuonyesha hali halisi, jinsi ndugu wanavyopaswa kuishi, wakati wote wanaposubiri kupata furaha kuu kuliko furaha zote na iliyo nje ya uwezo wao, ambayo si kutoka ndani mwao, na wala si kwa uwajibikaji wao , wala juhudi zao, ingawa yote hayo ni muhimu, lakini katika kushirikishana uaminifu wa Mungu , mwenye kujenga misingi yote ya hekalu ambalo ni Kanisa. Ni furaha na amani ambayo dunia haiwezi kuitoa lakini inatoka katika ahadi ya Bwana kwa wafuasi wake , Yesu Mfufuka , aliyowapatia kwa uwezo wafuasi wake kwa njia ya Roho Mtakatifu.
Baba Mtakatifu Francisco, aliendelea kusema, Mitume Petro na Andrea, walisikia ahadi hii , na kuipokea kama zawadi . Ndugu hawa katika kuzaliwa , walikutana na Yesu na kufanywa kuwa ndugu katika imani na huduma. Na hivyo ndivyo ilikuwa ni furaha kwao, kwa jioni hiyo , kushiriki kama ndugu katika Ibada hii ya sala za shukurani na Sifa kwa Mungu kama ndugu waliojawa na tumaini la Bwana Mfufuka. Ni neema ya kipekee na uwajibikaji , katika kutembea pamoja kwenye tumaini hili , wakidumishwa na kuimarishwa na maombezi ya Mitume na Watakatifu Petro na Andrea.
Kwa furaha hiyo, Papa alitoa shukurani zake za dhati na kuonyesha mategemeo mengi, kutoka kwa Mkuu wa kanisa la Constantinople na kwa Kanisa lote. Na aliwatakia kila la heri katika maadhimisho ya Siku Kuu ya Mtakatifu Andrea, na kuomba maomb ajili yake, na kwa Kanisa la Roma.
Baada ya Ibada hii, Patriaki Bartholomew I, na mgeni wake Papa Francisco walikutana katika hali ya faragha , katika chumba cha juu cha gorofa ya pili , ambamo pamoja na mazungumzano, pia walibadilishana zawadi na kutakia mema.
Jumamosi majira la jioni , Papa Francisco alishiriki katika sala ya Kiekumeni kama ilivyoandaliwa na Patriaki Bartholomew I, Mkuu wa Kanisa la Kiotodosi la Constatinople . Sala hiyo ilifanyika katika Kanisa Kuu la Kipatriaki la Mtakatifu George la Phanar.
Ibada hii ilipambwa kwa nyimbo wakati Papa na Patriaki walipoingia ndani ya Kanisa, ikifuatiwa na sala za masifu na shukurani kwa Mungu, pia yalitolewa maombi kuwaombea viongozi wa Kanisa ,Papa na Patriaki na kwa ajili ya Umoja wa Makanisa ya Mungu. Neno la Mungu lililosomwa kutoka Kitabu cha Zakaria 8, 7-17( “ Bwana Mungu wa Majeshi asema, Tazama , nitawaokoa watu wangu kutoka nchi ya Mashariki na toka Magharibi , nao nitawaleta ....”).
Baba Mtakatifu katika homilia yake, alirejea aya za Neno la Mungu kutoka Kitabu cha Nabii Zakaria , na kuomba neema ya Bwana iweze kuleta upya na kuwadumisha katika misingi ya kutembea pamoja siku hadi siku , wakiwa wameimarika katika mwamba wa furaha na matumaini. Msingi huo ni ahadi ya Bwana .
Papa alionyesha shukurani zake zao dhati kwa ndugu yake katika Bwana Bartholomew 1, kwa mapokezi na makaribisho mazuri yenye kuonyesha hali halisi, jinsi ndugu wanavyopaswa kuishi, wakati wote wanaposubiri kupata furaha kuu kuliko furaha zote na iliyo nje ya uwezo wao, ambayo si kutoka ndani mwao, na wala si kwa uwajibikaji wao , wala juhudi zao, ingawa yote hayo ni muhimu, lakini katika kushirikishana uaminifu wa Mungu , mwenye kujenga misingi yote ya hekalu ambalo ni Kanisa. Ni furaha na amani ambayo dunia haiwezi kuitoa lakini inatoka katika ahadi ya Bwana kwa wafuasi wake , Yesu Mfufuka , aliyowapatia kwa uwezo wafuasi wake kwa njia ya Roho Mtakatifu.
Baba Mtakatifu Francisco, aliendelea kusema, Mitume Petro na Andrea, walisikia ahadi hii , na kuipokea kama zawadi . Ndugu hawa katika kuzaliwa , walikutana na Yesu na kufanywa kuwa ndugu katika imani na huduma. Na hivyo ndivyo ilikuwa ni furaha kwao, kwa jioni hiyo , kushiriki kama ndugu katika Ibada hii ya sala za shukurani na Sifa kwa Mungu kama ndugu waliojawa na tumaini la Bwana Mfufuka. Ni neema ya kipekee na uwajibikaji , katika kutembea pamoja kwenye tumaini hili , wakidumishwa na kuimarishwa na maombezi ya Mitume na Watakatifu Petro na Andrea.
Kwa furaha hiyo, Papa alitoa shukurani zake za dhati na kuonyesha mategemeo mengi, kutoka kwa Mkuu wa kanisa la Constantinople na kwa Kanisa lote. Na aliwatakia kila la heri katika maadhimisho ya Siku Kuu ya Mtakatifu Andrea, na kuomba maomb ajili yake, na kwa Kanisa la Roma.
Baada ya Ibada hii, Patriaki Bartholomew I, NAMGENI WAKE Papa Francisco walikutana katika hali ya faragha , katika chumba cha juu cha gorofa ya pili , ambamo pamoja na mazungumzano, pia walibadilishana zawadi na kutakia mema.

All the contents on this site are copyrighted ©.