2014-11-29 10:58:16

Viongozi wa dini:Ni wajibu kukemea maovu dhidi ya ubinadamu..Papa

Baba Mtakatifu Francisco , Ijumaa, kama sehemu ya ratiba yake, alitembelea Idara ya Mambo ya Kidini “ Diyanet“ ya Ankra Uturuki. Diyanet, ni chombo cha kidini chenye kuwa na Mamlaka makubwa katika dhehebu la Waislamu Wasunni, ambao ni asilimia 68 ya Waislamu nchini Uturuki, Washiite wakiwa asilimia 30%. Idara hiyo ilianzishwa mwaka 1924, baada ya taifa kufuta utawala wa Kiislamu, kuwa taifa huria lisiloegemea dini yoyote.

Baba Mtakatifu Francisco katika hotuba yake kwa Ofisi ya Diyanet na Rais wake , Profesa Mehmet Gormez, alitoa shukurani zake za dhati kwa mwaliko wao, uliomwezesha kumpa nafasi ya kuwa na muda huu wa kushirikishana mawazo na viongozi wa kisiasa na kidini, wote Waislamu na Wakristo nchini Uturuki.

Na alishukuru kwamba, sasa umekuwa ni kama utamaduni kwa Mapapa , wakati wakitembelea nchini mbalimbali kama sehemu ya utume wao, kukutana pia na viongozi wa dini mbalimbali. Papa alisema, bila kuwa na uwazi huu kukutana na kuzungumza na watu mbalimbali, ziara yake kama Papa, madhumuni yake yangekuwa na upungufu. Kwa mtazamo huo,na kwa heshima, amekuwa na hamu ya kukutana na Rais wa Diyanet, akifuata nyayo za watangulizi wake. Alieleza na kurejesha kumbukumbu zake kwa namna ya kipekee kwa ziara ya Papa Benedict XVI, aliyoifanya Novemba 2006.

Baba Mtakatifu Francisco aliridhia kwamba, Uhusiano mzuri na mazungumzo kati ya viongozi wa dini, kwa kweli, yana umuhimu mkubwa. Na huwakilisha wazi ujumbe wa kushughulikiwa na jumuiya zao, ikionyesha yote mawili kuheshimiana na urafiki kwamba, inawezekana, licha ya tofauti za imani. Urafiki kama huo, pamoja na kuwa na muhimu wake wenyewe, huwa pia na maana kubwa, hasa pale panapotokea kutoelewana katika baadhi ya utendaji na kuzaa migogoro ile inayoshuhudiwa sasa katika baadhi ya nchi duniani, ambako yamekuwa ni maafa makubwa kwa watu wasiokuwa na hatia..

Papa aliendelea kuzungumzia athari za vita vyenye kusababisha vifo vya waathirika wasio na hatia na kuleta uharibifu mkubwa usioweza kuelezeka, ulio kinyume na maadili na dini, mvutano na migogoro, njaa na umaskini, na hata uharibifu wa mazingira ya asili - hewa, maji na ardhi.

Hotuba ya Papa ililenga katika hali ya kutisha ya vita Mashariki ya Kati, juu ya yote nchini Iraq na Syria, ambako kila mtu anateseka na hali mbaya ya maisha yasiyoweza kuelezeka kama matokeo ya migogoro ya kisiasa. Papa alipeleka mawazo yake kwa watoto wengi, mama wengi, wazee na wengine wengi wasioweza kujitetea, watu waliolazimika kukimbia makazi yao wakiwa tupu, wakipambanishwa na kila aina ya unyanyasaji, kama matokeo ya ubabe wa makundi ya watu wachache. Papa alionyesha kujali dhuluma hizi zinazo fanya na watu wenye ubinafsi wenye msimamo mkali, wenye kulazimisha itikadi zao kwa jamii nzima, na hasa wale wanaokataa kuongekea imani tofauti wasiosadiki, si tu Wakristo na Wayazidi, lakini pi ana makundi mengine madogomadogo yanayo endelea kuteswa vurugu za kinyama, sababu ya utambulisho wao wa kikabila na kidini. Vurugu ambazo si tu zinaondoa maisha ya watu lakini pia urithi wa maana wa majengo matakatifu, makaburi, alama za kidini na urithi wa kitamaduni, na kumbukumbu zingine muhimu kwa jamii.

Bada ya Maelezo Papa aliwageukia viongozi wa dini, kwamba, wana wajibu mkubwa kukemea wote wale wanaokiuka utu na haki za binadamu. Maisha ya binadamu, ni zawadi ya Mungu Muumba, na yana kila tabia takatifu. Hivyo ghasia na vurugu zozote zile zinazotafuta kuhalalisha dini kwa kuangamiza maisha ya watu ni zinapaswa kulaaniwa vikali, kwa sababu Mungu ni Mungu wa uzima na amani.

Dunia inatarajia kuona wale wanaotangaza habari za kumheshimu Mungu na kumwabudu , wake kwa waume, kuwa watu wa amani, wenye kuwa na uwezo wa kuishi na kuwapokea watu wote kama ndugu, bila kujali kabila, dini, utamaduni au kuwa na itikadi tofauti.

Na kwa ajili ya kukataa vurugu kama hizo, Papa Francisco aliongeza, ni lazima viongozi wa kidini kufanya kazi kwa pamoja nakupata majawabu ya pamoja kunapojitokeza migogoro. Hili linahitaji ushirikiano wa wote: Serikali, viongozi wa kisiasa na kidini, Wawakilishi wa asasi za kiraia na wanaume na wanawake wote wenye nia njema. Katika njia ya kipekee, viongozi wa dini wanaweza kutoa mchango wao muhimu kwa kuonyesha maadili ya mila zao. Papa alisema, viongozi Waislamu na Wakristo, ni viongozi wa hazina ya kiroho ambayo thamani yake haina makadirio. Katika hili, wanatambua kwamba, baadhi ya mambo wanayoshirikishana , ingawa kila mmoja anaishi kwa mujibu wa utamaduni wake , kama vile Ibada kwa Mungu mmoja pekee , rejea kwa Baba wa Imani Abraham, sala , sadaka na kufunga ... vipengele ambavyo wanaviishi kwa moyo wa kweli na huweza kubadilisha mfumo wa maisha na kuwa nguzo msingi ya uhakika katika kuheshimiana na udugu.

Na kwa kutambua na kuendeleza maendeleo ya urithi wa kawaida wa kiroho, kwa njia ya mazungumzo kati ya dini , husaidia kukuza na kutekeleza maadili, amani na uhuru katika jamii, kama alivyoeleza pia Mtakatifu Yohana Paulo wa II, katika hotuba yake kwa Jumuiya Katoliki , wakati alipotembelea Ankara, Novemba 29 1979. Utambuzi wa pamoja wa utakatifu wa kila maisha ya binadamu ni msingi wa juhudi za pamoja kwa ajili ya ujenzi wa mshikamano, matendo ya huruma, na ufanisi wa msaada, unaolengwa kutolewa kwa wale wanao teseka zaidi. Kwa ajili ya suala hili, Papa alitoa shukurani zake za kwa watu wote wa Uturuki, Waislamu na Wakristo sawia, kwa kuwapokea na kuwasaidia Mamia ya maelfu ya watu ambao wanakimbia nchi yao kwa migogoro. Papa alieleza na kutaja milioni watuhasa waliotoka Iraki na Syria. Ametaja kuwa ni mfano wa wazi wa jinsi gani, inawezekana kufanya kazi pamoja katika kuwahudumia watu wengine wahitaji Ni mfano wa kutia moyo, na unaohitaji kuimarishwa.

Mwisho wa hotuba yake, Papa, alionyesha kufurahia na kuridhika na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Diyanet na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Majadiliano na dini zingine. Na alitaja hamu yake inayolenga kuona kwamba, mahusiano haya yataendelea kuimarika na kuwa na nguvu kwa manufaa ya wote. Ii kwamba kila juhudi kwa ajili ya kukuza majadiliano halisi, ziweze kuwa ishara ya matumaini duniani, ambalo ni hitaji kuu kwa ajili ya uwepo wa amani , usalama na ustawi wa watu. Papa aliendelea kuonyesha matumaini yake kwamba, mkutano wake na Rais wa Diyanet, utaweza kufungua ukurasa mpya wa ubunifu wenye nguvu zaidi katika majadiliano kati ya dini.

Na alirudia kutoa shukurani zake kwa Raisi na ujumbe wake ulioshiriki katika mkutano huo ,akiwaombea mioyo yao ijazwe na furaha tele. Aidha alimshukuru kila mmoja kwa uwepo wake na kwa ajili ya maombezi yao, kwake yeye na kwa ajili ya huduma zake za Kitume. Na kwa upande wake , Papa aliwahakikishia sala zake, kuwatakia wote Baraza za Bwana.

Baba Mtakatifu Francisco , Ijumaa, kama sehemu ya ratiba yake, alitembelea Idara ya Mambo ya Kidini “ Diyanet“ ya Ankra Uturuki. Diyanet, ni chombo cha kidini chenye kuwa na Mamlaka makubwa katika dhehebu la Waislamu Wasunni, ambao ni asilimia 68 ya Waislamu nchini Uturuki, Washiite wakiwa asilimia 30%. Idara hiyo ilianzishwa mwaka 1924, baada ya taifa kufuta utawala wa Kiislamu, kuwa taifa huria lisiloegemea dini yoyote.

Baba Mtakatifu Francisco katika hotuba yake kwa Ofisi ya Diyanet na Rais wake , Profesa Mehmet Gormez, alitoa shukurani zake za dhati kwa mwaliko wao, uliomwezesha kumpa nafasi ya kuwa na muda huu wa kushirikishana mawazo na viongozi wa kisiasa na kidini, wote Waislamu na Wakristo.

Na alishukuru kwamba, sasa umekuwa ni kama utamaduni kwa Mapapa , wakati wakitembelea nchini mbalimbali kama sehemu ya utume wao, kukutana pia na viongozi wa dini mbalimbali. Papa alisema, bila kuwa na uwazi huu kukutana na kuzungumza na watu mbalimbali, ziara yake kama Papa, madhumuni yake yangekuwa na upungufu. Kwa mtazamo huo, pia kwa heshima, amekuwa na hamu ya kukutana na Rais wa Diyanet, akifuata nyayo za watangulizi wake na alikumbuka kwa namna ya kipekee ziara ya Papa Benedict XVI, aliyoifanya Novemba 2006.

Baba Mtakatifu Francisco aliridhia kwamba, Uhusiano mzuri na mazungumzo kati ya viongozi wa dini, kwa kweli, yana umuhimu mkubwa. Na huwakilisha wazi ujumbe wa kushughulikiwa na jumuiya zao, ikionyesha yote mawili kuheshimiana na urafiki kwamba vinawezekana, licha ya tofauti za imani. Urafiki kama huo, pamoja na kuwa na muhimu wake wenyewe, huwa pia na maana kubwa, hasa pale panapotokea kutoelewana katika baadhi ya utendaji na kuzaa migogoro ile inayoshuhudiwa sasa katika baadhi ya nchi duniani, ambako yamekuwa ni maafa makubwa kwa watu wasiokuwa na hatia..

Papa aliendelea kuzungumzia athari za vita vyenye kusababisha vifo vya waathirika wasio na hatia na kuleta uharibifu mkubwa usioweza kuelezeka, ulio kinyume na maadili na dini, mvutano na migogoro, njaa na umaskini, na hata uharibifu wa mazingira ya asili - hewa, maji na ardhi.

Hotuba ya Papa ililenga katika hali ya kutisha ya vita Mashariki ya Kati, juu ya yote nchini Iraq na Syria, ambako kila mtu anateseka na hali mbaya ya maisha yasiyoweza kuelezeka kama matokeo ya migogoro y kisiasa. Papa alipeleka mawazo yake kwa watoto wengi, mateso ya mama wengi, wazee na wengine wengi wasioweza kujitetea, watu waliolazimika kukimbia makazi yao wakiwa tupu, wakipambanishwa na kila aina ya unyanyasaji, kama matokeo ya ubabe wa makundi ya watu wachache. Papa alionyesha kujali dhuluma hizi zinazo fanya na watu wenye ubinafsi wenye msimamo mkali, wenye kulazimisha itikadi zao kwa jamii nzima, na hasa wale wanaokataa kuongekea imani tofauti wasiosadiki, si tu Wakristo na Wayazidi, lakini pi ana makundi mengine madogomadogo yanayo endelea kuteswa vurugu za kinyama, sababu ya utambulisho wao wa kikabila na kidini. Vurugu ambazo si tu zinaondoa maisha ya watu lakini pia urithi wa maana wa majengo matakatifu, makaburi, alama za kidini na urithi wa kitamaduni, na kumbukumbu zingine muhimu kwa jamii.

Bada ya Maelezo Papa aliwageukia viongozi wa dini, kwamba, wana wajibu mkubwa kukemea wote wale wanaokiuka utu na haki za binadamu. Maisha ya binadamu, ni zawadi ya Mungu Muumba, na yana kila tabia takatifu. Hivyo ghasia na vurugu zozote zile zinazotafuta kuhalalisha dini kwa kuangamiza maisha ya watu ni zinapaswa kulaaniwa vikali, kwa sababu Mungu ni Mungu wa uzima na amani.
Dunia inatarajia kuona wale wanaotangaza habari za kumheshimu Mungu na kumwabudu , wake kwa waume, kuwa watu wa amani, wenye kuwa na uwezo wa kuishi na kuwapokea watu wote kama ndugu, bila kujali kabila, dini, utamaduni au kuwa na itikadi tofauti.

Na kwa ajili ya kukataa vurugu kama hizo, Papa Francisco aliongeza, ni lazima viongozi wa kidini kufanya kazi kwa pamoja nakupata majawabu ya pamoja kunapojitokeza migogoro. Hili linahitaji ushirikiano wa wote: Serikali, viongozi wa kisiasa na kidini, Wawakilishi wa asasi za kiraia na wanaume na wanawake wote wenye nia njema. Katika njia ya kipekee, viongozi wa dini wanaweza kutoa mchango wao muhimu kwa kuonyesha maadili ya mila zao. Papa alisema, viongozi Waislamu na Wakristo, ni viongozi wa hazina ya kiroho ambayo thamani yake haina makadirio. Katika hili, wanatambua kwamba, baadhi ya mambo wanayoshirikishana , ingawa kila mmoja anaishi kwa mujibu wa utamaduni wake , kama vile Ibada kwa Mungu mmoja pekee , rejea kwa Baba wa Imani Abraham, sala , sadaka na kufunga ... vipengele ambavyo wanaviishi kwa moyo wa kweli na huweza kubadilisha mfumo wa maisha na kuwa nguzo msingi ya uhakika katika kuheshimiana na udugu.

Na kwa kutambua na kuendeleza maendeleo ya urithi wa kawaida wa kiroho, kwa njia ya mazungumzo kati ya dini , husaidia kukuza na kutekeleza maadili, amani na uhuru katika jamii, kama alivyoeleza pia Mtakatifu Yohana Paulo wa II, katika hotuba yake kwa Jumuiya Katoliki , wakati alipotembelea Ankara, Novemba 29 1979. Utambuzi wa pamoja wa utakatifu wa kila maisha ya binadamu ni msingi wa juhudi za pamoja kwa ajili ya ujenzi wa mshikamano, matendo ya huruma, na ufanisi wa msaada, unaolengwa kutolewa kwa wale wanao teseka zaidi. Kwa ajili ya suala hili, Papa alitoa shukurani zake za kwa watu wote wa Uturuki, Waislamu na Wakristo sawia, kwa kuwapokea na kuwasaidia Mamia ya maelfu ya watu ambao wanakimbia nchi yao kwa migogoro. Papa alieleza na kutaja milioni watuhasa waliotoka Iraki na Syria. Ametaja kuwa ni mfano wa wazi wa jinsi gani, inawezekana kufanya kazi pamoja katika kuwahudumia watu wengine wahitaji Ni mfano wa kutia moyo, na unaohitaji kuimarishwa.

Mwisho wa hotuba yake, Papa, alionyesha kufurahia na kuridhika na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Diyanet na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Majadiliano na dini zingine. Na alitaja hamu yake inayolenga kuona kwamba, mahusiano haya yataendelea kuimarika na kuwa na nguvu kwa manufaa ya wote. Ii kwamba kila juhudi kwa ajili ya kukuza majadiliano halisi, ziweze kuwa ishara ya matumaini duniani, ambalo ni hitaji kuu kwa ajili ya uwepo wa amani , usalama na ustawi wa watu. Papa aliendelea kuonyesha matumaini yake kwamba, mkutano wake na Rais wa Diyanet, utaweza kufungua ukurasa mpya wa ubunifu wenye nguvu zaidi katika majadiliano kati ya dini.

Na alirudia kutoa shukurani zake kwa Raisi na ujumbe wake ulioshiriki katika mkutano huo ,akiwaombea mioyo yao ijazwe na furaha tele. Aidha alimshukuru kila mmoja kwa uwepo wake na kwa ajili ya maombezi yao, kwake yeye na kwa ajili ya huduma zake za Kitume. Na kwa upande wake , Papa aliwahakikishia sala zake, kuwatakia wote Baraza za Bwana.

All the contents on this site are copyrighted ©.