2014-11-28 15:45:08

Vyombo vya habari kamwe visiwe visima vya uchochezi na ghasia.


Baba Mtakatifu Francisco Alhamis alikutana na familia ya Mtakatifu Paulo ambao ni mashuhuri katika uwanja wa habari na mawasiliano. Wawakilishi wa Familia hii ya Mtakatifu Paulo ambao kwa kifupi hujulikana kama Wapaolini, walimtembelea Papa Francisco kama sehemu ya hija yao katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. kwa ajili ya kutimia miaka mia ya kuanzishwa kwa shirika lao na Mwenye Heri Giacomo Alberione.
Papa katika hotuba yake kwa Wapaolini, aliwaambia Wakristo wote kwamba, wana jukumu la kutangaza Injili , bila ya kubagua mtu. Na kwamba ,maadhimisho ya miaka mia, aliongeza Papa ni fursa nyingine mpya, ya kufanya upya imani katika maisha na mawasiliano, hasa kwa njia ya zana uchapishaji na vyombo mbalimbali vya mawasiliano.

Watu watu wote na wajishughulishe na kutangaza habari njema ya kwamba Mungu ni upendo. Na kwa maneno ya Yesu, "Uhuru mmepokea bure , toeni bure", Papa aliitaja aya hii kuwa ni siri ya uinjilishaji. Kwamba, kuiwasilisha Injili , katika mtindo wake wa kiinjili, ni neema ya bure, bila kuitokea jasho. Ni kiinua mgongo kwa Mkristo, hasa muumini anaye pokea kwa furaha na upendo safi na kuiwasilisha zawadi hii ya upendo kwa wengine, kupitia huduma, Ukarimu na upendo.

Hata hivyo, Papa aliongoza, ni tu kwa kufanya kazi kwa furaha, kunakoweza kutengeneza mawasiliano ya kweli miongoni mwa watu. Ni vigumu kuwasilisha neno la furaha iwapo anayewasilisha halifurahii neno hilo. Na ndiyo maana wale walio pokea ujumbe wa Injili kwa furaha wanaweza kuiwasilisha furaha hiyo kwa wengine. Mawasiliano mazuri ni mzizi wa mafanikio ya kukua kiroho, Papa alieleza na kurejea Waraka wake wa Kichungaji wa Injili ya Furaha (Evangelii gaudium, 9).

Kuinjilisha, kimsingi, ni kutangaza Injili "kwa wale ambao hawajui Yesu Kristo au kwa wale wanaoikataa. Kwa msukumo huo, Papa Francisco alisisitiza kuwa , inakuwa ni haki ya kila Mkristo kuitangaza Injili bila kumbagua mtu .Na kwao Wapaolini , kama Wakatoliki, DNA ya damu yao, inapaswa kuwa ukatoliki, kama ilivyokuwa kwa mwanzilishi wa shirika lao, wakivuviwa na maisha na utume wa Mtakatifu Paulo.
Papa aliendelea kulitaja Kanisa kuwa ni mfano wa Msafiri, mwenye kuonyesha tumaini lake kwa Kristo.
Wakristo ni Kanisa hujaji, ambalo mizizi wake ni kumtangaza Kristo na upendo wake kwa viumbe wote, kufungua vifundo vyote vya pingu za mitindo ya maisha ya kidunia, na kuweka wazi roho na uwezo wa mitazamo na matukio kwa neema ya Bwana.

Ujumbe wa Papa unasema, bado kuna wengi wanasubiri kumjua Yesu Kristo. Ndoto ya upendo usiojua mipaka isipokuwa kufungua barabara mpya kuleta pumzi mpya ya Injili katika tamaduni na katika maeneo mbalimbali ya jamii.Huu ni wito wa kitume kwa ajili ya wogofu wa mtu binafsi na jamii . Na ni tu mioyo iliyo wazi katika kuipokea neema hii ya mahusiano inayoweza kupata uelewa na maana ya ishara za nyakati na kutoa wito katika hitaji la kibinadamu, matumaini na amani.

Alikamilisha kwa kuwalenga Wapaolini akisema , katika njia yao ya kumfuata Kristo na kwa ushuhuda wao, ni wazi Mwaka kwa ajili ya Maisha yaliyowekwa Wakfu utaweza kuwa msaada Mkubwa katika maisha yao ya kitawa na katika kulitumikia kanisa na dunia kwa ujumla.Papa alieleza na kuwatakia baraka za Bwana katika shughuli zao za kila siku.








All the contents on this site are copyrighted ©.