2014-11-24 15:23:23

Ni kazi ya Kanisa kutangaza kwa bidii ukweli wa Mwanga unaomlikia Maisha bora...Papa


Kwa unyenyekevu, umaskini na uaminifu kwa Kristo, Kanisa huutangaza mwanga unaomlika katika maisha bora zaidi, ingawa hupambana na majaribu ya lenyewe kutiwa giza giza katika kuuonyesha mwanga unaoimulikia dunia kwa Mungu. Baba Mtakatifu alieleza hili wakati wa homilia yake ya mapema Jumatatu hii,akiwa katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican.
Papa alisema, Kanisa hujitangaza kwa bidii hadharani, kwa sababu ndani yake mna utajiri mkubwa wa imani na matumiani, yenye kulishwa na neema na katika kuwa macho dhidi ya ubatili. Ni wito wake kutoa kila lilicho nacho, bila ya kujali imani ya mtu kwa Mungu. Papa alieleza kwa kutazama mfano ulitolewa katika somo la Injili, juu ya mwanamke mjane maskini, ambaye kwa unyenyekevu anatoa sadaka fedha yote aliyokuwa nayo, senti mbili, katika mfuko wa hazina, kinyume na matajiri walioweka kiasi kikubwa cha fedha, lakini fedha hiyo ilikuwa ni ziada katika utajiri wao.

Papa Francisco amesema hizi ni tabia mbili ambazo huambatana na Kanisa muda wote wa historia yake, kwamba, neema ya Kanisa hujaribiwa na ubatili na umaskini. Na hivyo kwa Kanisa, inadai na ni lazima na muhimu, kutumia busara na hekima, katika kuona utendaji mbalimbali wa waumini wake bila kujali hadhi yao kijamii. Yesu anasifu sadaka ya mwanamke mjane kwamba, ni kuu kuliko sadaka ya matajiri, majne anatoa senti za mwisho alizokuwa nazo, ambapo matajiri wanatoa kilichokuwa cha ziada katika mifuko yao, hivyo matajiri hawa hawakupungukiwa na chochote, fedha hiyo , ilikuwa ni ziada katika fungu zima la utajiri waliokuwa nao, tofauti na mwanamke mjane aliyetoa tena kwa unyenyekevu kila kitu alichona.

Papa alitafakari mfano huu akisema, mwanamke huyu mjane, hakuwa na umaarufu wowote kwa jamii na ndani ya Kanisa kwa kuwa hakuwa na utajiri wowote. Wengi hawakuvutiwa hata na imani yake ya ndani. Kwa macho ya wengi, mchango wake wa senti mbili ulikuwa si kitu , wala kuwa na maana yoyote, hata kutangazwa. Lakini kumbe kwa macho ya Mungu yanayoona nia zote za ndani, amekuwa ni muhimu kuliko matajiri walioweka kiasi kikubwa kutoka katika ziada ya utajiri wao.

Papa aliianisha sura mwanamke huyo mjane na Kanisa, akisema, Kanisa katika hali ya umaskini, wakati likimsubiri kurudi kwa mara ya pili, bwana harusi wake , linapaswa kuonyesha upendo na fadhila kubwa, kwa kutumia kile kidogo lililocho nacho, kuhudumia wengine.Ni lazima mwanga wake mdogo, uangaze juu yake lenyewe, na hatimae kuwa mwanga mkubwa katika utendaji na haki na fadhila.

Bwana amekwisha tangaza kwamba, kazi ya Kanisa ni kuangazia ubinadamu, mwanga Kristo ambao kila mmoja ameupokea katika ubatizo, kwa unyenyekevu, kuhudumia wote, na kupitia huduma hizi mwanga huo wa kanisa upate kuonekana duniani kote. Papa alieleza na kusema , huduma yoyote ile isiyomulikiwa na mwanga huu, haifai kitu. Na alifahamisha kwamba, Kanisa halitoi huduma kwa wahitaji kwa sababu ni tajiri, au lina nguvu, au kwa ajili ya kutazama yaliyojitokeza katika historia yake, au kile kinachotokea katika maisha ya waamini wake, lakini Kanisa hulenga katika kuwa mwanga kwa wengine, katika maana ya kuonyesha hasa mahali alipo Bwana, ambaye yeye Mwenyewe ndiye Mwanga.
Wakati Kanisa linatenda kwa uaminifu na matumaini kwa Bwana arusi wake, Papa Francisco alirudia kusema mara kwa mara, kwa furaha ya hupokea mwanga kutoka kwa Bwana wake, kama ilivyokuwa kwa mwanamke mjane, kwa imani na matumaini. Kanisa huendelea kusubiri kwa unyenyekevu , hata pale linapokabiliwa na shida na taabu na kupungukiwa na kuwa maskini, waaamini wote wanapaswa kubaki aminifu. Mfano huu wa Mjane, unalifundisha Kanisa kutoa kila kitu lililonacho kwa ajili ya wengine , kwa kuwa kila jambo na kila kitu ni kwa ajili ya Bwana na kwa ajili ya wengine. Kanisa hutenda kwa unyenyekevu, bila kujigamba, matanuzi wala fahali, ila tu kwa ajili ya kuuwezesha mwanga wake uonekane kwa wengine. Daima ni kuutafuta mwanga, Mwanga unaotoka kwa Bwana Yesu Kristo, na kuufikisha mwanga huo kwa wengine.








All the contents on this site are copyrighted ©.