Serikali ya mpito Burkina Faso yaanza kazi kwa makeke!
Rais Michel Kafando wa Burkina Faso na Luteni Kanali Isaac Zida, Waziri mkuu wameanza
kutekeleza dhamana ya kuliongoza Taifa katika kipindi cha mpito, kuelekea uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2015, kwa kula kiapo cha utii, Ijumaa, tarehe
22 Novemba 2014. Viongozi hawa wamefikisha kikomo cha uongozi wa Rais Blaise Compaorè
alitebwaga mwanyanga hivi karibuni kwa kuhofia nguvu ya umma baada ya jaribio la kutaka
kupindisha Katiba ya nchi ili aendelee kubaki madarakani kushindikana.
Rais
Kafando kwa miaka kumi na mitano amekuwa ni Mwakilishi wa kudumu wa Burkina Faso kwenye
Umoja wa Mataifa na amewahi pia kuwa ni Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano
wa kimataifa. Katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa Rais Kafando ameahidi kuanza
mchakato wa kukomesha rushwa na ufisadi wa mali ya umma, ili kuhakikisha kwamba, haki
inatendeka pamoja na kuwa n auhakika wa mahali ambapo Rais Thomas Sankara, aliyejitwalia
madaraka kunako mwaka 1983 na baadaye kupinduliwa na Bwana Blaise Compaorè, aliyekuwa
rafiki yake wa karibu mwaka mmoja baadaye.
Bwana Compaorè kwa sasa amekimbilia
uhamishoni huko Morocco baada ya kuondoka Pwani ya Pembe ambako anashutumiwa kujihusisha
katika machafuko yaliyojitokeza nchini humo hivi karibuni.