2014-11-23 09:27:50

Kanisa limempoteza kiongozi mahiri!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa Bwana Vinicio Angelini, kufuatia kifo cha Kardinali Fiorenzo Angelini, Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma za kichungaji kwa wafanyakazi katika sekta ya afya kilichotokea Jumamosi, tarehe 22 Novemba 2014 mjini Roma.

Baba Mtakatifu anapenda kutuma salam zake za rambi rambi kwa wote walioguswa na kifo cha Kardinali Angelini, kiongozi aliyechangia kwa kiasi kikubwa ustawi na maendeleo ya Kanisa katika ujumla wake; akishiriki katika huduma za maisha ya kiroho kwa Chama cha Vijana Wakatoliki; Mhudumu wa shughuli za kiroho hospitalini na hatimaye, Rais wa Baraza la Kipapa la huduma za kichungaji kwa wafanyakazi katika sekta ya afya.

Baba Mtakatifu Francisko anasema kwa maombezi ya Bikira Maria afya watu wa Roma, ampokee Mtumishi hodari na Kiongozi wa Kanisa katika raha na amani ya milele. Anapenda kuomboleza na wale wanaoomboleza pamoja na kuwapatia baraka zake za kitume!

Naye Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anapenda kuungana na ndugu, jamaa na wote wanaoomboleza kifo cha Kardinali Fiorenzo Angelini na kwamba, anamwombea ili aweze kupata pumziko la milele kwa ulinzi na tunza ya Bikira Maria. Anawashukuru watawa waliomhudumia Kardinali Angelini katika maisha yake.







All the contents on this site are copyrighted ©.