2014-11-23 14:28:27

Jengeni na kudumisha moyo wa ushirikiano na maridhiano kwa jili ya mafao ya wengi!


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Siku kuu ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu sanjari na kuwatangaza watakatifu wapya sita, aliwashukuru wawakilishi kutoka katika nchi wanamotoka watakatifu hawa kwa kushiriki katika Ibada ya Misa Takatifu, lakini zaidi amewataka wananchi wa Italia kujenga na kudumisha moyo wa ushirikiano na mapatano kwa ajili ya mafao ya wengi, huku wakionesha matumaini kwa kesho iliyo bora pamoja na kutumainia uwepo wa Mungu ambaye daima amekuwa karibu nao na kamwe hawezi kuwaacha katika nyakati ngumu za maisha.

Kwa watakatifu wawili wanaotoka India, nchi ambayo ni chemchemi kubwa ya miito ya kipadre na kitawa, Mwenyezi Mungu asaidie kuleta mwamko mpya wa Kimissionari kwa Kanisa nchini India, kwa kujikita katika maridhiano na upatanisho, ili Wakristo nchini India waweze kusonga mbele katika hija ya mshikamano na maisha ya kidugu. Familia yote ya Mungu imewekwa chini ya ulinzi na usimamizi wa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa, Malkia wa Watakatifu na mfano wa Wakristo.







All the contents on this site are copyrighted ©.