2014-11-22 07:30:02

Sherehe ya Kristo Mfalme na Watakatifu wapya!


Katika maadhimisho ya Sherehe ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu, Jumapili asubuhi, tarehe 23 Novemba 2014, Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican pamoja na kuwatangaza Wenyeheri sita kuwa Watakatifu.

Hawa ni Mwenyeheri Giovanni Antonio Farina, Askofu; Kuriakose Elias CHavara wa Familia Takatifu, Padre; Ludovico wa Casoria, Padre; Nicola wa Longobardi, Mtawa, Aufrasia Eluvathingal wa Moyo Mtakatifu wa Yesu pamoja na Mwenyeheri Amato Ronconi, Mtawa, Utawa wa Tatu wa Mtakatifu Francisko.

Kanisa linasherehekea Siku kuu ya Yesu Kristo Mfalme wa mbingu na dunia, enzi na utawala vyote ni vyake, changamoto na mwaliko kwa Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema kuhakikisha kwamba, wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu unaosimikwa katika: ukweli na uzima; Utakatifu na Neema; Haki, Mapendo na Amani.








All the contents on this site are copyrighted ©.