2014-11-22 08:13:07

Kikosi kazi cha maadhimisho ya Sinodi ya kawaida ya Maaskofu, 2015


Kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu, itakayofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 25 Oktoba 2015, kwa kuongozwa na kauli mbiu "Wito na Utume wa Familia katika Kanisa na Ulimwengu mamboleo", Baba Mtakatifu amewateuwa Makardinali wafuatao kuwa ni Marais wawakilishi wakati wa maadhimisho hayo.

Hawa ni:
1. Kardinali Andrè Vingt-Trois, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Paris, Ufaransa.
2. Kardinali Luis Antonio G. Tagle, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Manila, Ufilippini.
3. Kardinali Raymundo Damasceno Assis, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Aparecida
4. Kardinali Wilfrid Fox Napier, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini.

Baba Mtakatifu amemteua Kardinali Peter Erdò, Askofu mkuu wa Esztetgom, Budapest, kuwa ni Msimamizi mkuu wa Sinodi ya Maaskofu; Askofu mkuu Bruno Forte kutoka Jimbo kuu la Chieti Vasto kuwa Katibu mkuu maalum wa Sinodi ya kawaida ya Maaskofu kwa ajili ya familia.







All the contents on this site are copyrighted ©.